The chat will start when you send the first message.
1Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu;
Unilinde uhai wangu kutoka kwa hofu ya adui.
2Unifiche mbali na njama za watenda mabaya,[#Zab 143:9]
Mbali na mipango ya watu wafanyao maovu;
3Waliounoa ulimi wao kama upanga,[#Zab 57:4]
Wanaoyalenga maneno ya uchungu kama mishale,
4Wapate kumpiga mkamilifu faraghani,
Kwa ghafla humpiga bila kuogopa.
5Walijifanya hodari katika jambo baya;
Hushauriana juu ya kutega mitego;
Wakisema, Ni nani atakayeiona?
6Ni nani atambuaye maovu yetu?
Tumepanga njama kwa werevu mwingi,
Maana katika moyo wa mtu na fikira nyingi zimefichika.
7Lakini Mungu atawapiga kwa mshale wake,
Na kuwajeruhi ghafla.
8Kwa ajili ya ulimi wao wataangamizwa;[#Mit 12:13]
Wote wawaonao watatetemeka kwa hofu.
Wote wawaonao watatikisa kichwa.
9Na watu wote wataogopa,
Wataitangaza kazi ya Mungu,
Na kuyafahamu matendo yake.
10Mwenye haki atamfurahia BWANA na kumkimbilia,[#Zab 32:11; Flp 4:4]
Na wote wenye moyo wa adili watasifu.