The chat will start when you send the first message.
1Wafilisti walipopigana nao Waisiraeli, watu wa Isiraeli wakawakimbia Wafilisti kwa madonda waliyopigwa, wakaanguka, wakafa kule mlimani kwa Gilboa.
2Wafilisti wakawafuata na kuandamana na Sauli na wanawe, Wafilisti wakawaua wana wa Sauli: Yonatani na Abinadabu na Malkisua.
3Mapigano yakawa makali hapo, Sauli alipokuwa; wapiga mishale walipomwona, akaumizwa nao wapiga mishale.
4Ndipo, Sauli alipomwambia mchukua mata yake: Uchomoe upanga wako, unichome nao, hao wasiotahiriwa wasije kunichezea vibaya! Mchukua mata yake alipokataa kwa kuogopa sana, Sauli akausimika upanga, akauangukia.
5Mchukua mata yake alipoona, ya kuwa Sauli amekufa, naye akauangukia upanga wake, akafa.
6Ndivyo, Sauli alivyokufa na wanawe watatu, nao wa mlango wake wote wakafa pamoja naye.
7Watu wote wa Isiraeli waliokaa kule katika mbuga ya bondeni walipoona, ya kuwa wamekimbizwa, ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao wakakimbia nao; kisha Wafilisti wakaja, wakakaa humo.
8Ikawa kesho yake, Wafilisti walipokuja kuwapambua waliouawa, wakamwona Sauli na wanawe, jinsi walivyokufa mlimani kwa Gilboa.
9Wakampambua, wakakichukua kichwa chake na mata yake, wakatuma wajumbe kwenda po pote katika nchi ya Wafilisti kuyatangaza penye vinyago vyao, hata kwa watu.
10Mata yake wakayaweka nyumbani mwa mungu wao, nacho kichwa chake wakakiangika kwa misumari nyumbani mwa Dagoni.
11Watu wote wa Yabesi wa Gileadi walipoyasikia yote, Wafilisti waliyomfanyizia Sauli,
12wakaondoka watu wote walioweza kupiga vita, wakauchukua mzoga wa Sauli, nayo mizoga ya wanawe, wakaipeleka Yabesi, wakaizika mifupa yao chini ya mkwaju kwao Yabesi, wakafunga mfungo siku saba.[#2 Sam. 2:5.]
13Ndivyo, Sauli alivyokufa kwa kumvunjia Bwana maagano, aliyoyafanya naye, kwa kuwa hakulishika Neno la Bwana, tena kwa kuwa alitafuta mwaguaji aliyejua kukweza mizimu.[#1 Sam. 15:11; 28:8.]
14Kwa kuwa hakutaka kuongozwa na Bwana, akamwua, nao ufalme akauondoa kwake, akampa Dawidi, mwana wa Isai.