Mashangilio 134

Mashangilio 134

Kumtukuza Mungu na usiku.

1Mtukuzeni Bwana, nyote mlio watumishi wa Bwana, msimamao na usiku Nyumbani mwake Bwana!

2Iinueni mikono yenu hapo Patakatifu! Mtukuzeni Bwana!

3Bwana akubariki toka Sioni, yeye aliyeziumba mbingu na nchi![#Sh. 115:15; 128:5.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania