The chat will start when you send the first message.
1Israeli alipokuwa mtoto, nilikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri.[#Kut 4:22; Mt 2:15]
2Kadiri walivyowaita ndivyo walivyoondoka na kuwaacha; waliwatolea dhabihu Mabaali, na kuzifukizia uvumba sanamu za kuchonga.[#2 Fal 17:16]
3Lakini nilimfundisha Efraimu kwenda kwa miguu; niliwachukua mikononi mwangu; hawakujua ya kuwa niliwaponya.[#Isa 46:3; Kut 15:26]
4Niliwavuta kwa kamba za kibinadamu, kwa mafungo ya upendo; nami nilikuwa kwao kama hao waondoao kongwa tayani mwao, nikaandaa chakula mbele yao.[#Zab 78:25]
5Hatarudi tena nchi ya Misri; bali huyo Mwashuri atakuwa mfalme wake; kwa sababu walikataa kurejea.[#2 Fal 17:13; Yer 8:4-6; Hos 6:1; Amo 4:6; Zek 1:4]
6Na upanga utaiangukia miji yake, utayaharibu makomeo yake na kuyala, kwa sababu ya mashauri yao wenyewe.
7Na watu wangu wamejipinda kuniacha; ingawa wawaita kwenda kwake Aliye Juu, hapana hata mmoja atakayemtukuza.
8Niwezeje kukuacha, Efraimu? Niwezeje kukuachilia Israeli? Niwezeje kukufanya kama Adma? Niwezeje kukuweka kama Seboimu? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja.[#Yer 9:7; Mwa 19:25; Yer 31:20; Kum 29:23]
9Sitatumia ukali wa hasira yangu, sitamwangamiza Efraimu tena; kwa maana mimi ni Mungu, si mwanadamu mimi; mimi ndiye aliye Mtakatifu katikati yenu; wala sitaingia ndani ya mji.[#Hes 23:19; Isa 55:8,9; Mal 3:6; Rum 11:19]
10Watakwenda kumfuata BWANA, atakayenguruma kama simba; kwa maana atanguruma, nao watoto watakuja kutoka magharibi wakitetemeka.
11Watakuja wakitetemeka kama shomoro, toka Misri, na kama hua, toka nchi ya Ashuru; nami nitawakalisha katika nyumba zao, asema BWANA.
12Efraimu amenizunguka kwa maneno ya uongo, na nyumba ya Israeli kwa udanganyifu; na Yuda hata sasa anasitasita kwa Mungu, na kwake aliye Mtakatifu, naye ni mwaminifu.