The chat will start when you send the first message.
1Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo;
Uliniokoa nilipokuwa katika shida;
Unifadhili na kuisikia sala yangu.
2Enyi wanadamu, hadi lini utukufu wangu utafedheheka?
Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo hadi lini?
3Bali jueni ya kuwa BWANA amejiteulia mtauwa;[#Kut 33:16; 2 Pet 2:9]
BWANA husikia nimwitapo.
4Muwe na hofu wala msitende dhambi,[#Efe 4:26; Mit 3:7]
Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
5Toeni dhabihu za haki,[#Kum 33:19; Zab 37:3]
Na kumtumaini BWANA.
6Wengi husema, Nani atakayetuonesha mema?[#Zab 80:3]
BWANA, utuinulie nuru ya uso wako.
7Umenitia furaha moyoni mwangu,
Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.
8Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara,[#Law 26:5; Kum 12:10; Yn 14:27; Flp 4:7]
Maana Wewe, BWANA, peke yako,
Ndiwe unijaliaye kukaa salama.