Wagalatia 4

Wagalatia 4

1LAKINI nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, ajapokuwa bwana wa yote;

2bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hatta muhulla uliokwisha kuamriwa na baba.

3Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.

4Hatta ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwana wake, amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sharia,

5illi awakomboe waliokuwa chini ya sharia, tupate kupokea hali ya wana.

6Na kwa kuwa ninyi ni wana, Mungu alimtuma Roho ya Mwana wake mioyoni mwenu, aliaye, Abba, Baba.

7Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali mwana; na kama u mwana, bassi, u mrithi wa Mungu kwa Kristo.

8Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkujua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu.

9Bali sasa, mkiisha kumjua Mungu, ya nini kurejea tena kwa mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge na yenye upungufu ambayo mnataka kuyatumikia tena.

10Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka.

11Nawachelea, isiwe labda nimejitaabisha burre kwenu.

12Nakusihini, ndugu, mwe kama mimi, maana mimi kama ninyi. Hamkunidhulumu neno.

13Lakini mwajua ya kuwa naliwakhubiri Injili marra ya kwanza kwa sababu ya ndhaifu wa mwili;

14na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Yesu Kristo.

15Ku wapi, bassi, kule kujiita kheri? Maana nawashuhudia, kwamba, kama ingaliwezekana, mngaliugʼoa macho yenu, mkanipa mimi.

16Bassi, je! nimekuwa adui wenu kwa sababu nawa ambieni yaliyo kweli?

17Wao wawaonea uinyi shauku lakini si kwa vema bali wanataka kuwafungia mlango illi ninyi mwaonee wao shauku.

18Na ni vyema kuonewa shauku katika neno jema siku zote, wala si wakati nikiwapo mimi tu.

19Vitoto vyangu, ambao nawaonea utungu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu.

20Naam, ningependa kuwa pamoja nanyi sasa, na kuigeuza santi yangu; maana nawaonea maashaka.

21Niambieni, ninyi ninaotaka kuwa chini ya sharia, hamwisikii torati?

22Kwa maana, imeandikwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili, mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana.

23Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi.

24Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio maagano mawili, moja toka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ndio Hajir.

25Maana Hajir ni mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemi wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto wake.

26Bali Yerusalemi wa juu ni mwungwana, ndio mama yetu sisi.

27Kwa maana imeandikwa,

Fanya furaha, tassa usiyezaa;

Paaza sauti, ukalie, wewe usiye na utungu;

Kwa sababu watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko wake aliye na mume.

28Sisi, ndugu, kama Isaak, tu watoto wa ahadi.

29Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alimwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, vivyo hivyo na sasa.

30Lakini lanenani Andiko? Mtupe nje mjakazi na mwana wake, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana.

31Kwa hiyo, ndugu, sisi si watoto wa mjakazi, hali wake aliye mwungwana.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania