Yakobo 4

Yakobo 4

1VITA na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humo, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?

2Mwatamani, wala hanma kitu; mwana na kuona wivu, na hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi.

3Mwaomba wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, illi mvilumie kwa tamaa zenu.

4Enyi wazinzi, wanaume na wanawake, hamjui ya kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? bassi killa atakae kuwa rafiki wa dunia ajifanya kuwa adui wa Mungu.

5Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema burre? Roho ikaayo ndani yetu hutamani kiasi cha kuona wivu?

6Lakini atupa sisi neema nyingi zaidi; kwa hiyo asema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neemi wanyenyekevu.

7Bassi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, nae atawakimbia.

8Mkaribieni Mungu, nae atsiwakaribieni ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, kaisafisheni mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.

9Jihuzunisheni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu kugeuzwe kuwa kuomboleza na furaha yenu kuwa hamu.

10Jidhilini mbele za Bwana, nae atawakuzeni.

11Msisingiziane, ndugu; amsingiziae ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, aisingizia sharia na kuihukumu sharia. Lakini ukiihukumu sharia, huwi mtenda sharia, bali mhukumu.

12Mtoa sharia na mbukumu ni mmoja tu, awezae kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umbukumuye mwenzako?

13Haya bassi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia mji fullani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; nanyi hamjui yatakayokuwa kesho.

14Uzima wenu ni nini? Maana ninyi moshi uonekanao kwa kitambo, kiisha hutoweka.

15Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hayi na kufanya hivi au hivi.

16Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kwote kwa namna hii ni kubaya.

17Bassi yeye ajuae kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyu ni dhambi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania