The chat will start when you send the first message.
1Kisha Bildadi, Mshuhi, akajibu:
2“Mungu ni mwenye uwezo mkuu,
watu wote na wamche.
Yeye huweka amani mpaka juu kwake mbinguni.
3Nani awezaye kuhesabu majeshi yake?
Ni nani asiyeangaziwa na mwanga wake?
4Mtu awezaje basi, kuwa mwadilifu mbele ya Mungu?
Binadamu tu awezaje kujidai kuwa safi?
5Kwake Mungu, hata mwezi haungai vya kutosha;
nyota nazo si safi mbele yake;
6sembuse mtu ambaye ni mdudu,
binadamu ambaye ni buu tu!”