The chat will start when you send the first message.
1Nakutazamia kwa hamu, ee Mwenyezi-Mungu,
nakuangalia wewe utawalaye huko juu mbinguni!
2Kama watumishi wamtegemeavyo bwana wao,
kama mjakazi amtegemeavyo bibi yake,
ndivyo nasi tunavyokutegemea wewe,
ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,
mpaka hapo utakapotuonea huruma.
3Utuhurumie, ee Mwenyezi-Mungu, utuhurumie,
maana tumedharauliwa kupita kiasi.
4Tumeshiba muda mrefu dharau za matajiri,
tumepuuzwa mno na wenye kiburi.