The chat will start when you send the first message.
1Wapumbavu hujisemea moyoni:[#Rom 3:10-12]
“Hakuna Mungu!”
Wote wamepotoka kabisa,
wametenda mambo ya kuchukiza;
hakuna hata mmoja atendaye jema.
2Mungu anawaangalia wanadamu kutoka mbinguni,
aone kama kuna yeyote mwenye busara,
kama kuna yeyote anayemtafuta Mungu.
3Lakini wote wamekosa,
wote wamepotoka pamoja,
hakuna atendaye mema,
hakuna hata mmoja.
4“Je, hao watendao maovu hawana akili?
Wanawatafuna watu wangu kama mikate;
wala hawanijali mimi Mungu!”
5Hapo watashikwa na hofu kubwa,
hofu ambayo hawajapata kuiona;
maana Mungu ataitawanya mifupa ya adui,
hao wataaibika maana Mungu amewakataa.
6Laiti ukombozi wa Israeli ungefika kutoka Siyoni!
Mungu atakaporekebisha hali ya watu wake,
wazawa wa Yakobo watashangilia;
Waisraeli watafurahi.