The chat will start when you send the first message.
1Mungu amejenga mji wake
juu ya mlima wake mtakatifu.
2Mwenyezi-Mungu anaupenda mji wa Siyoni,
kuliko makao mengine ya Yakobo.
3Mambo ya fahari yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu:
4“Miongoni mwa wale wanijuao mimi,
wapo watu wa Misri na Babuloni.
Kadhalika Filistia, Tiro na Kushi,
wote walizaliwa kwako!”
5Na kuhusu Siyoni itasemwa:
“Siyoni ni mama wa huyu na huyu;
Mungu Mkuu atauthibitisha.”
6Mwenyezi-Mungu ataandika katika kitabu,
atakapoorodhesha watu:
“Huyu amezaliwa huko!”
7Wote wanacheza ngoma na kuimba:
“Siyoni, chanzo chetu ni kwako.”