The chat will start when you send the first message.
1Mwenyezi-Mungu anatawala;
amejivika fahari kuu!
Mwenyezi-Mungu amevaa fahari na nguvu!
Ameuimarisha ulimwengu, nao hautatikisika kamwe.
2Kiti chako cha enzi ni imara tangu kale;
wewe umekuwapo kabla ya nyakati zote.
3Vilindi vimetoa sauti, ee Mwenyezi-Mungu;
naam, vimepaza sauti yake,
vilindi vyapaza tena mvumo wake.
4Mwenyezi-Mungu ana enzi kuu juu mbinguni,
ana nguvu kuliko mlio wa bahari,
ana nguvu kuliko mawimbi ya maji.
5Ee Mwenyezi-Mungu, maagizo yako ni thabiti;
nyumba yako ni takatifu milele na milele.