1 Nyakati 23

1 Nyakati 23

Jamaa za Walawi na utendaji wao

1Daudi alipokuwa mzee aliyeshiba siku, akamfanya Sulemani mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli.

2Pia akawakusanya viongozi wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.

3Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa elfu thelathini na nane.

4Daudi akasema, “Miongoni mwa hawa, elfu ishirini na nne watasimamia kazi ya Hekalu la Bwana na elfu sita watakuwa maafisa na waamuzi,

5na elfu nne watakuwa mabawabu, na wengine elfu nne watamsifu Bwana kwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.”

Wagershoni

7Wana wa Wagershoni walikuwa wawili:

8Wana wa Ladani walikuwa watatu:

9Wana wa Shimei walikuwa watatu:

10Nao wana wa Shimei walikuwa:

Wakohathi

12Wana wa Kohathi walikuwa:

13Wana wa Amramu walikuwa:

15Wana wa Musa walikuwa:

16Wazao wa Gershomu:

17Wazao wa Eliezeri:

18Wana wa Ishari:

19Wana wa Hebroni walikuwa:

20Wana wa Uzieli walikuwa:

Wamerari

21Wana wa Merari walikuwa:

Wana wa Mahli walikuwa:

23Wana wa Mushi:

28Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Haruni kuhudumu katika Hekalu la Bwana : Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu.

29Walikuwa wasimamizi wa mikate iliyowekwa mezani, unga kwa ajili ya sadaka za nafaka, mikate myembamba isiyotiwa chachu, uokaji na uchanganyaji, pamoja na vipimo vyote vya wingi na ukubwa.

30Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana . Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni

31na wakati wowote sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa Bwana siku za Sabato na kwenye sikukuu za Mwezi Mwandamo na katika sikukuu nyingine zilizoamriwa. Iliwapasa kuhudumu mbele za Bwana mara kwa mara kwa idadi maalum na kwa namna waliyokuwa wamepewa maelekezo.

32Hivyo Walawi wakafanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, katika Mahali Patakatifu chini ya uongozi wa ndugu zao wazao wa Haruni, kwa ajili ya utumishi katika Hekalu la Bwana .

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.