The chat will start when you send the first message.
1Mwenyezi Mungu amwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
hadi nitakapowafanya adui zako
kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
2Mwenyezi Mungu ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;
utatawala katikati ya adui zako.
3Askari wako watajitolea kwa hiari
katika siku yako ya vita.
Ukiwa umevikwa fahari takatifu,
kutoka tumbo la mapambazuko
utapokea umande wa ujana wako.
4Mwenyezi Mungu ameapa,
naye hatabadilisha mawazo yake:
“Wewe ni kuhani milele,
kwa mfano wa Melkizedeki.”
5Bwana yuko mkono wako wa kuume,
atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.
6Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga
na kuwaponda watawala wa dunia nzima.
7Atakunywa maji katika kijito kando ya njia;[#110:7 au Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka;]
kwa hiyo atainua kichwa chake juu.