The chat will start when you send the first message.
1Mwenyezi Mungu asipoijenga nyumba,
wajengao hufanya kazi bure.
Mwenyezi Mungu asipoulinda mji,
walinzi wakesha bure.
2Mnajisumbua bure kuamka mapema
na kuchelewa kulala,
mkitaabikia chakula:
kwa maana yeye huwapa usingizi wapendwa wake.
3Watoto ni urithi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu,
uzao ni zawadi kutoka kwake.
4Kama mishale mikononi mwa shujaa
ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.
5Heri mtu ambaye podo lake
limejazwa nao.
Hawataaibishwa wanaposhindana
na adui zao langoni.