The chat will start when you send the first message.
1Heri wale wote wamchao Mwenyezi Mungu,
wanaoenda katika njia zake.
2Utakula matunda ya kazi yako;
baraka na mafanikio vitakuwa vyako.
3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao
ndani ya nyumba yako;
wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni
kuizunguka meza yako.
4Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa
mtu amchaye Mwenyezi Mungu.
5Mwenyezi Mungu na akubariki kutoka Sayuni
siku zote za maisha yako,
na uone mafanikio ya Yerusalemu,
6nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako.
Amani iwe juu ya Israeli.