Zaburi 13

Zaburi 13

Zaburi 13

Sala ya kuomba msaada

1Hadi lini, Ee Bwana ? Je, utanisahau milele?

Utanificha uso wako hadi lini?

2Nitapambana na mawazo yangu hadi lini,

na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu?

Adui zangu watanishinda hadi lini?

3Nitazame, unijibu, Ee Bwana Mungu wangu.

Yatie nuru macho yangu,

ama sivyo nitalala usingizi wa mauti.

4Adui yangu atasema, “Nimemshinda,”

nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.

5Lakini ninategemea upendo wako usiokoma;

moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.

6Nitamwimbia Bwana ,

kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.