The chat will start when you send the first message.
1Dunia ni mali ya Bwana , na vyote vilivyomo,
ulimwengu, na wote wanaoishi ndani yake,
2maana aliiwekea misingi yake baharini,
na kuifanya imara juu ya maji.
3Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana ?
Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?
4Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe,
yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake
au kuapa kwa kitu cha uongo.
5Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana ,
na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.
6Hiki ndicho kizazi cha wale wanaomtafuta,
wale wanaoutafuta uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
7Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
inukeni enyi milango ya kale,
ili mfalme wa utukufu apate kuingia.
8Ni nani huyu Mfalme wa utukufu?
Ni Bwana aliye na nguvu na uweza,
ni Bwana aliye hodari katika vita.
9Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
viinueni juu enyi milango ya kale,
ili Mfalme wa utukufu apate kuingia.
10Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu?
Ni Bwana wa majeshi;
yeye ndiye Mfalme wa utukufu.