The chat will start when you send the first message.
1Ee Bwana , nithibitishe katika haki,
maana nimeishi maisha yasiyo na lawama;
nimemtumainia Bwana
bila kusitasita.
2Ee Bwana , unijaribu, unipime,
uuchunguze moyo wangu
na mawazo yangu;
3kwa maana upendo wako
uko mbele yangu daima,
nami natembea siku zote
katika kweli yako.
4Siketi pamoja na watu wadanganyifu,
wala siandamani na wanafiki,
5ninachukia kusanyiko la watenda maovu,
na ninakataa kuketi pamoja na waovu.
6Ninanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia,
naikaribia madhabahu yako, Ee Bwana ,
7nikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa,
huku nikisimulia matendo yako ya ajabu.
8Ee Bwana , naipenda nyumba yako unakoishi,
mahali pale utukufu wako hukaa.
9Usiiondoe nafsi yangu pamoja na watenda dhambi,
wala uhai wangu pamoja na wanaomwaga damu,
10ambao mikononi mwao kuna mipango miovu,
ambao mikono yao ya kuume imejaa rushwa.
11Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama;
nikomboe na unihurumie.
12Miguu yangu imesimama katika uwanja tambarare;
katika kusanyiko kuu nitamsifu Bwana .