The chat will start when you send the first message.
1Nijibu nikuitapo,
Ee Mungu wangu mwenye haki!
Nipumzishe katika shida zangu;
nirehemu, usikie ombi langu.
2Enyi watu, mtabadilisha utukufu wangu
kuwa aibu hadi lini?
Mtapenda udanganyifu
na kufuata miungu ya uongo hadi lini?
3Fahamuni hakika kwamba Bwana amewatenga
wale wamchao kwa ajili yake;
Bwana atanisikia nimwitapo.
4Katika hasira yako, usitende dhambi.
Tulieni kimya mkiwa vitandani mwenu,
mkiichunguza mioyo yenu.
5Toeni dhabihu zilizo haki;
mtegemeeni Bwana .
6Wengi wanauliza, “Ni nani awezaye
kutuonesha jema lolote?”
Ee Bwana , tuangazie nuru ya uso wako.
7Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa
kuliko watu waliopata nafaka na divai kwa wingi.
8Nitajilaza chini na kulala kwa amani,
kwa kuwa wewe peke yako, Ee Bwana ,
waniwezesha kukaa kwa salama.