The chat will start when you send the first message.
1Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa;
Ee Bwana , njoo hima unisaidie.
2Wale wanaotafuta kuniua,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu.
3Wale wanaoniambia, “Aha! Aha!”
na warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
4Lakini wote wanaokutafuta
washangilie na kukufurahia,
wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme,
“Bwana ni mkuu!”
5Lakini mimi bado ni maskini na mhitaji;
Ee Mungu, unijie haraka.
Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;
Ee Bwana , usikawie.