The chat will start when you send the first message.
1Bwana anatawala, amejivika utukufu;
Bwana amejivika utukufu
tena amejivika nguvu.
Dunia imewekwa imara,
haitaondoshwa.
2Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;
wewe umekuwa tangu milele.
3Bahari zimepaza, Ee Bwana ,
bahari zimepaza sauti zake;
bahari zimepaza sauti za mawimbi yake.
4Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,
ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:
Bwana aishiye juu sana ni mkuu.
5Ee Bwana , sheria zako ni imara;
utakatifu umepamba nyumba yako
pasipo mwisho.