The chat will start when you send the first message.
1Haya ni maneno yaliyoandikwa na Baruku mwana wa Neria, mjukuu wa Maaseya, wa ukoo wa Sedekia, Hasadia na Hilkia. Baruku aliandika haya huko Babuloni
2mnamo siku ya saba ya mwezi katika mwaka wa tano baada ya Wakaldayo kuuteka mji wa Yerusalemu na kuuteketeza.[#1:2 Labda ni mwezi wa tano katika kalenda ya Kiebrania (taz 2 Fal 25:8; Yer 52:12).]
3Baruku aliyasoma maneno haya aliyoandika mbele ya mfalme Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, na mbele ya watu wote waliokuja kusikiliza,[#1:3 Jina lingine la Yoakimu (taz Yer 22:24).]
4na mbele ya wakuu na wana wa wafalme, na wazee; aliyasoma mbele ya watu wote, wakubwa kwa wadogo, ambao waliishi huko Babuloni pande za mto Sudi.
5Baada ya kuyasikia, waliomboleza, wakafunga chakula na kuomba dua kwa Bwana.
6Kisha wakachanga fedha, kila mtu akatoa kadiri ya uwezo wake,
7wakizipeleka Yerusalemu kwa kuhani Yoakimu mwanawe Hilkia, na mjukuu wa Shalumu, na kwa makuhani wengine pamoja na watu wote waliokuwa pamoja naye huko Yerusalemu.
8Siku ya kumi ya mwezi wa Siwani, Baruku alitwaa vyombo vitakatifu vilivyokuwa vimetolewa katika nyumba ya Mungu, akavirudisha nchini Yuda. Vyombo hivyo vya fedha vilikuwa vimetengenezwa na mfalme Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda,
9baada ya Nebukadneza mfalme wa Babuloni kumwondoa mfalme Yekonia huko Yerusalemu na kumpeleka Babuloni yeye pamoja na wakuu, wafungwa, wenye mamlaka na watu wengine wa kawaida.[#1:9 Hivyo Kigiriki; labda mafundi.]
10Basi, watu waliandika hivi:
15Hivi ndivyo mtakavyosema:
“Bwana Mungu wetu ni mwadilifu, lakini sisi tulivyo leo tumejaa aibu! Sisi sote, watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu,
16wafalme wetu, wakuu wetu, makuhani wetu, manabii wetu na wazee wetu.
17Sisi tumetenda dhambi dhidi ya Bwana.
18Tulimwasi, wala hatukutii sauti ya Bwana Mungu wetu aliposema tuishi kufuatana na amri alizotupa sisi.
19Tangu siku ile Bwana alipowatoa wazee wetu nchini Misri mpaka leo, tumeendelea kukosa utii kwa Bwana Mungu wetu, tukawa wazembe kuhusu jambo la kusikia sauti yake.
20Kwa hiyo, mpaka leo hii tumekabiliwa na balaa na laana zile alizotamka Mose mtumishi wa Bwana kwa amri yake, siku ile alipowatoa wazee wetu nchini Misri ili kutupa nchi inayotiririka maziwa na asali.
21Sisi hatukusikiliza maneno ya manabii ambao Bwana Mungu wetu aliwatuma kwetu.
22Badala yake, kila mmoja wetu amepania kufuata mipango ya moyo wake mwovu, kwa kutumikia miungu mingine na kufanya yaliyo maovu mbele ya Bwana Mungu wetu.