1 Mambo 1

Vizazi vya baba toka Adamu hata Isaka.

1Adamu, Seti, Enosi,[#1 Mose 5.]

2Kenani, Mahalaleli, Yaredi,[#1 Mose 10:2-5.]

3Henoki, Metusela, Lameki,

4Noa, Semu, Hamu na Yafeti.

5Wana wa Yafeti: Gomeri na Magogi na Madai na Yawani na Tubali na Meseki na Tirasi.

6Nao wana wa Gomeri: Askenazi na Rifati na Togarma.

7Nao wana wa Yawani: Elisa na Tarsisa, Wakiti na Wadodani.

8Wana wa Hamu: Kusi na Misri, Puti na Kanaani.[#1 Mose 10:6-20.]

9Nao wana wa Kusi: Seba na Hawila na Sabuta na Rama na Sabuteka. Nao wana wa Rama: Saba na Dedani.

10Naye Kusi akamzaa Nimurodi; ndiye aliyeanza kuwa mwenye nguvu katika nchi.

11Naye Misri akawazaa Waludi na Waanami na Walehabi na Wanafutuhi

12na Wapatirusi na Wakasiluhi, ambao Wafilisti walitoka kwao, na Wakafutori.

13Naye Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hiti;

14tena Myebusi na Mwamori na Mgirgasi,

15na Mhiwi na Mwarki na Msini,

16na Mwarwadi na Msemari na Mhamati.

17Wana wa Semu: Elamu na Asuri na Arpakisadi na Ludi na Aramu na Usi na Huli na Geteri na Meseki.[#1 Mose 10:21-31.]

18Naye Arpakisadi akamzaa Sela, naye Sela akamzaa Eberi.

19Naye Eberi akazaliwa wana wawili: jina lake wa kwanza ni Pelegi (Gawanyiko), kwa kuwa siku zake ndipo, nchi hii ilipogawanyika; nalo jina la nduguye ni Yokitani.

20Naye Yokitani akamzaa Almodadi na Selefu na Hasarmaweti na Yera,

21na Hadoramu na Uzali na Dikla,

22na Ebali na Abimaeli na Saba,

23na Ofiri na Hawila na Yobabu; hawa wote ndio wana wa Yokitani.

24Semu, Arpakisadi, Sela,[#1 Mose 11:10-26; 1 Mambo 1:17.]

25Eberi, Pelegi, Reu,

26Serugi, Nahori, Tera,

27Aburamu naye ndiye Aburahamu.

28Wana wa Aburahamu ni Isaka na Isimaeli.

29Navyo vizazi vyao ni hivi: Mwanawe wa kwanza wa Isimaeli ni Nebayoti, tena Kedari na Adibeli na Mibusamu,[#1 Mose 16:15; 21:3; 1 Mose 25:13-16.]

30Misima na Duma, Masa, Hadadi na Tema,

31Yeturi, Nafisi na Kedima. Hawa ndio wana wa Isimaeli.

32Nao wana wa Ketura, suria yake Aburahamu, ni hawa: Akamzaa Zimurani na Yokisani na Medani na Midiani na Isibaki na Sua. Nao wana wa Yokisani ni Saba na Dedani.[#1 Mose 25:1-3.]

33Nao wana wa Midiani ni Efa na Eferi na Henoki na Abida na Eldaa. Hawa wote ndio wana wa Ketura.

34Kisha Aburahamu akamzaa Isaka; nao wana wa Isaka ni Esau na Isiraeli.[#1 Mose 25:19-26.]

Wana wa Esau na wafalme wa Edomu.

35Wana wa Esau: Elifazi, Reueli na Yeusi na Yalamu na Kora.[#1 Mose 36:10-19.]

36Wana wa Elifazi: Temani na Omari na Sefi na Gatamu, Kenazi na Timuna na Amaleki.

37Wana wa Reueli: Nahati, Zera, Sama na Miza.

38Nao wa Seiri: lotani na Sobali na Siboni na Ana na Disoni na Eseri na Disani.[#1 Mose 36:20-30.]

39Nao wana wa Lotani: Hori na Homamu, naye umbu lake Lotani ni Timuna.

40Wana wa Sobali: Aliani na Manahati na Ebali, Sefi na Onamu. Nao wana wa Siboni ni Aya na Ana.

41Wana na Ana: Disoni, nao wana wa Disoni: Hamurani na Esibani na Itirani na kerani.

42Wana wa Eseri: Bilihani na Zawani na Yakani. Wana wa Disoni: Usi na Arani.

43Nao hawa ndio wafalme walioshika ufalme katika nchi ya Edomu, wana wa Isiraeli walipokuwa hawajapata bado mfalme: Bela, mwana wa Beori; nalo jina la mji wake ni Dinihaba.[#1 Mose 36:31-43.]

44Bela alipokufa, Yobabu, mwana wa Zera aliyetoka Bosira, akawa mfalme mahali pake.

45Yobabu alipokufa, Husamu wa nchi ya Watemani akawa mfalme mahali pake.

46Husamu alipokufa, Hadadi, mwana wa Bedadi aliyewapiga Wamidiani katika mbuga za Wamoabu, akawa mfalme mahali pake; nalo jina la mji wake ni Awiti.

47Hadadi alipokufa, Samula aliyetoka Masireka akawa mfalme mahali pake.

48Samula alipokufa, Sauli aliyetoka Rehoboti wa Mtoni akawa mfalme mahali pake.

49Sauli alipokufa, Baali-Hanani, mwana wa Akibori, akawa mfalme mahali pake.

50Baali-Hanani alipokufa, Hadadi akawa mfalme mahali pake, nalo jina la mji wake ni Pai; nalo jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matiredi, binti Mezahabu.

51Hadadi alipokufa, wakawa majumbe wa Edomu jumbe Timuna, jumbe Alia, jumbe Yeteti,

52jumbe Oholibama, jumbe Ela, jumbe Pinoni,

53jumbe Kenazi, jumbe Temani, jumbe Mibusari,

54jumbe Magidieli, jumbe Iramu; hawa ndio waliokuwa majumbe wa Edomu.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania