1 Mambo 3

Wana wa Dawidi na wafalme wa Yuda.

1Wana wa Dawidi, aliozaliwa Heburoni, walikuwa hawa: Wa kwanza Amunoni wa Mwizireeli Ahinoamu; wa pili Danieli wa Mkarmeli Abigaili;[#2 Sam. 3:2-5.]

2wa tatu Abisalomu, mwana wa Maka, binti Talmai, mfalme wa Gesuri; wa nne Adonia, mwana wa Hagiti;

3wa tano Sefatia wa Abitali; wa sita Itiramu wa mkewe Egla.

4Hawa sita ndio aliozaliwa Heburoni, alimokuwa mfalme miaka saba na miezi sita; lakini Yerusalemu alikuwa mfalme miaka thelatini na mitatu.

5Namo Yerusalemu alizaliwa hawa: Simea na Sobabu na Natani na Salomo; hawa wanne ni wa Bati-Sua, binti Amieli.[#2 Sam. 5:14-16; 1 Mambo 14:4-7.]

6Tena Ibuhari na Elisama na Elifeleti

7na Noga na Nefegi na Yafia

8na Elisama na Eliada na Elifeleti, ni tisa.

9Hawa ni wana wote wa wakeze Dawidi pasipo wana wa masuria; naye Tamari alikuwa umbu lao.[#2 Sam. 13:1.]

10Naye mwana wa Salomo ni Rehabeamu, mwanawe ni Abia, mwanawe ni Asa, mwanawe ni Yosafati,[#Mat. 1:7-12.]

11mwanawe ni Yoramu, mwanawe ni Ahazia, mwanawe ni Yoasi,

12mwanawe ni Amasia, mwanawe ni Azaria, mwanawe ni Yotamu,

13mwanawe ni Ahazi, mwanawe ni Hizikia, mwanawe ni Manase,

14mwanawe ni Amoni, mwanawe ni Yosia.

15Nao wana wa Yosia: wa kwanza ni Yohana, wa pili Yoyakimu, wa tatu Sedekia, wa nne Salumu.

16Nao wana wa Yoyakimu ni mwanawe Yekonia, mwanawe ni Sedekia.

17Nao wana wa Yekonia aliyetekwa ni mwanawe Saltieli,[#2 Mambo 36:10.]

18na Malkiramu na Pedaya na Senasari na Yekamia na Hosama na Nedabia.

19Nao wana wa Pedaya: Zerubabeli na Simei. Nao wana wa Zerubabeli: Mesulamu na Hanania na umbu lao Selomiti;

20tena Hasuba na Oheli na Berekia na Hasadia na Yusabu-Hesedi, watu watano.[#Ezr. 3:2,8.]

21Nao wana wa Hanania: Pelatia na Yesaya. Tena wana wa Refaya, wana wa Arnani, wana wa Obadia na wana wa Sekania.

22Nao wana wa Sekania: Semaya; nao wana wa Semaya: Hatusi na Igali na Baria na Naria na Safati, watu sita.

23Nao wana wa Naria: Eliyoenai na Hizikia na Azirikamu, watu watatu.

24Nao wana wa Eliyoenai: Hodawia na Eliasibu na Pelaya na Akubu na Yohana na Delaya na Anani, watu saba.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania