1 Mambo 6

Vizazi vya Lawi.

1Wana wa Lawi: Gersoni, Kehati na Merari.[#1 Mambo 6:16,18.]

2Nao wana wa Kehati: Amuramu, Isihari na Heburoni na Uzieli.[#1 Mambo 6:50-53; 2 Mose 6:20,23,25.]

3Nao wana wa Amuramu: Haroni na Mose na Miriamu; nao wana wa Haroni: Nadabu na Abihu, Elazari na Itamari.

4Elazari akamzaa Pinehasi, Pinehasi akamzaa Abisua.

5Naye Abisua akamzaa Buki, naye Buki akamzaa Uzi.

6Naye Uzi akamzaa Zeraya, naye Zeraya akamzaa Merayoti.

7Merayoti akamzaa Amaria, naye Amaria akamzaa Ahitubu.

8Naye Ahitubu akamzaa Sadoki, naye Sadoki akamzaa Ahimasi.[#2 Sam. 8:17; 15:27,36.]

9Naye Ahimasi akamzaa Azaria, naye Azaria akamzaa Yohana.

10Naye Yohana akamzaa Azaria; huyu ndiye aliyekuwa mtambikaji katika Nyumba hiyo, Salomo aliyoijenga Yerusalemu.

11Azaria akamzaa Amaria, naye Amaria akamzaa Ahitubu.

12Naye Ahitubu akamzaa Sadoki, naye Sadoki akamzaa Salumu.

13Naye Salumu akamzaa Hilkia, naye Hilkia akamzaa Azaria.[#2 Fal. 22:4.]

14Naye Azaria akamzaa Seraya, naye Seraya akamzaa Yosadaki.[#2 Fal. 25:18; Ezr. 7:1; Neh. 12:26.]

15Naye Yosadaki ndiye aliyekwenda nao Wayuda na Wayerusalemu, Bwana alipowahamisha kwa mkono wa Nebukadinesari.[#2 Fal. 25:21.]

16Wana wa Lawi: Gersomu, Kehati na Merari.

17Nayo haya ndiyo majina ya wana wa Gersomu: Libuni na Simei.[#2 Mose 6:16-19; 1 Mambo 6:1.]

18Nao wana wa Kehati: Amuramu na Isihari na Heburoni na Uzieli.

19Wana wa Merari: Mahali na Musi; huu ndio ukoo wao Walawi kwa milango ya baba zao.

20Wagersomu: Mwanawe Libuni, mwanawe huyo Yahati, mwanawe huyo Zima,

21mwanawe huyo Yoa, mwanawe huyo Ido, mwanawe huyo Zera, mwanawe huyo Yatiri.

22Wana wa Kehati: Mwanawe Aminadabu, mwanawe huyo Kora, mwanawe huyo Asiri,[#2 Mose 6:24.]

23mwanawe huyo Elkana, mwanawe huyo Ebiasafu, mwanawe huyo Asiri,

24mwanawe huyo Tahati, mwanawe huyo Urieli, mwanawe huyo Uzia, mwanawe huyo Sauli.

25Nao wana wa Elkana: Amasai na Ahimoti;

26mwanawe huyo Elkana, wanawe yeye Elkana: mwanawe Sofai, naye mwanawe huyo Nahati,

27mwanawe huyo Eliabu, mwanawe huyo Yerohamu, mwanawe huyo Elkana, (mwanawe huyo Samweli).[#1 Sam. 1:1.]

28Nao wana wa Samweli: Mzaliwa wa kwanza (Yoeli), tena wa pili Abia.[#1 Sam. 8:2.]

29Wana wa Merari: Mahali, mwanawe huyo Libuni, mwanawe huyo Simei, mwanawe huyo Uza,

30mwanawe huyo Simea, mwanawe huyo Hagia, mwanawe huyo Asaya.

Waimbaji wa Kilawi.

31Hawa ndio, Dawidi aliowaweka kwa ajili ya kuimba Nyumbani mwa Bwana, lile Sanduku lilipokuwa limekwisha kutua.

32Nao walikuwa wakitumika mbele ya Kao la Hema la Mkutano kwa kuimba, mpaka Salomo alipoijenga Nyumba ya Bwana mle Yerusalemu, wakasimama katika kazi zao na kupokeana zamu kama desturi yao.

33Nao hao ndio waliosimama katika kazi zao nao wana wao miongoni mwa wana wa Kehati: Mwimbishaji Hemani, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,[#1 Mambo 15:17.]

34mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elieli, mwana wa Toa,

35mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahati, mwana wa Amasai,

36mwana wa Elkana, mwana wa Yoeli, mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,

37mwana wa Tahati, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,

38mwana wa Isihari, mwana wa Kehati, mwana wa Lawi, mwana wa Isiraeli.

39Naye ndugu yake Asafu alisimama kuumeni kwake; Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Simea,[#1 Mambo 15:17.]

40mwana wa Mikaeli, mwana wa Basea, mwana wa Malkia,

41mwana wa Etini, mwana wa Zera, mwana wa Adaya,

42mwana wa Etani, mwana wa Zima, mwana wa Simei,

43mwana wa Yahati, mwana wa Gersomu, mwana wa Lawi.

44Nako kushotoni walisimama ndugu zao wana wa Merari: Etani, mwana wa Kisi, mwana wa Abudi, mwana wa Maluki,[#1 Mambo 15:17.]

45mwana wa Hasabia, mwana wa Amasia, mwana wa Hilkia,

46mwana wa Amusi, mwana wa Bani, mwana wa Semeri,

47mwana wa Mahali, mwana wa Musi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.

Walawi waliotumikia Nyumbani mwa Mungu.

48Ndugu zao Walawi wengine walikuwa wamepewa kazi zote za utumishi wa Kao la Nyumba ya Mungu.

49Naye Haroni na wanawe walikuwa wakivukiza hapo pa kuteketezea ng'ombe za tambiko napo hapo pa kuvukizia, tena walizifanya kazi zote za hapo Patakatifu Penyewe, wawapatie Waisiraeli upozi wakifanya yote, kama Mose, mtumishi wa Mungu, alivyowaagiza.[#2 Mose 28:1; 3 Mose 16.]

50Nao hawa ndio wana wa Aroni: Mwanawe Elazari, mwanawe huyo Pinehasi, mwanawe huyo Abisua,[#1 Mambo 6:3-8.]

51mwanawe huyo Buki, mwanawe huyo Uzi, mwanawe huyo Zeraya,

52mwanawe huyo Merayoti, mwanawe huyo Amaria, mwanawe huyo Ahitubu,

53mwanawe huyo Sadoki, mwanawe huyo Ahimasi.

Miji ya Walawi.

(54-81: Yos. 21.)

54Nayo haya ndiyo makao yao, walikotua katika mipaka yao: miongoni mwao wana wa Haroni ukoo wao Wakehati walipatwa na kura ya kwanza,

55kwa hiyo wakawapa Heburoni katika nchi ya Yuda pamoja na malisho yake yaliyouzunguka.

56Lakini mashamba ya huo mji na vijiji vyake wakampa Kalebu, mwana wa Yefune.

57Tena wakawapa wana wa Haroni miji ya kukimbilia ya Heburoni, tena Libuna pamoja na malisho yake na Yatiri na Estemoa pamoja na malisho yake

58na Hileni pamoja na malisho yake na Debiri pamoja na malisho yake

59na Asani pamoja na malisho yake na Beti-Semesi pamoja na malisho yake.

60Tena katika shina la Benyamini Geba pamoja na malisho yake na Alemeti pamoja na malisho yake na Anatoti pamoja na malisho yake. Miji yao yote ilikuwa 13 kwa hesabu ya koo zao.

61Nao wana wa Kehati waliosalia walipewa miji 10 kwa kupigiwa kura katika ukoo wa hilo shina (Efuraimu), tena katika nusu ya shina la nusu ya Manase.[#1 Mambo 6:66-70.]

62Nao wana wa Gersomu walipewa miji 13, iwe ya ukoo wao katika shina la Isakari na katika shina la Aseri na katika shina la Nafutali na katika shina la Manase huko Basani.[#1 Mambo 6:71-76.]

63Nao wana wa Merari walipewa kwa kupigiwa kura miji 12, iwe ya ukoo wao katika shina la Rubeni na katika shina la Gadi na katika shina la Zebuluni.[#1 Mambo 6:77-81.]

64Ndivyo, wana wa Isiraeli walivyowapa Walawi hiyo miji pamoja na malisho yao.

65Wakawapa kwa kuipigia kura ile miji, iliyotajwa majina yao katika shina la wana wa Yuda na katika shina la wana wa Simeoni na katika shina la wana wa Benyamini.[#1 Mambo 6:55-60.]

66Nao wengine waliokuwa wa ukoo wa wana wa Kehati walipata miji katika shina la Efuraimu, iwe yao.

67Wakawapa miji ya kukimbilia ya Sikemu pamoja na malisho yake milimani kwa Efuraimu, tena Gezeri pamoja na malisho yake

68na Yokimamu pamoja na malisho yake na Beti-Horoni pamoja na malisho yake

69na Ayaloni pamoja na malisho yake na Gati-Rimoni pamoja na malisho yake.

70Tena katika nusu ya shina la Manase Aneri pamoja na malisho yake na Bileamu pamoja na malisho yake. Hii ilikuwa yao wengine wa ukoo wa wana wa Kehati waliosalia.

71Wana wa Gersomu walipata katika ukoo wao wa nusu ya shina la Manase Golani ulioko Basani pamoja na malisho yake na Astaroti pamoja na malisho yake.

72Tena katika shina la Isakari: Kedesi pamoja na malisho yake na Daberati pamoja na malisho yake

73na Ramoti pamoja na malisho yake na Anemu pamoja na malisho yake.

74Tena katika shina la Aseri: Masali pamoja na malisho yake na Abudoni pamoja na malisho yake

75na Hukoki pamoja na malisho yake na Rehobu pamoja na malisho yake.

76Tena katika shina la Nafutali: Kedesi wa Galili pamoja na malisho yake na Hamoni pamoja na malisho yake na Kiriataimu pamoja na malisho yake.

77Wana wa Merari waliosalia walipata katika shina la Zebuluni: Rimoni pamoja na malisho yake na Tabori pamoja na malisho yake;

78tena ng'ambo ya pili ya Yordani kuelekea Yeriko upande wa Yordani wa maawioni kwa jua katika shina la Rubeni: Beseri wa nyikani pamoja na malisho yake na Yasa pamoja na malisho yake

79na Kedemoti pamoja na malisho yake na Mefati pamoja na malisho yake.

80Tena katika shina la Gadi: Ramoti wa Gileadi pamoja na malisho yake na Mahanaimu pamoja na malisho yake

81na Hesiboni pamoja na malisho yake na Yazeri pamoja na malisho yake.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania