The chat will start when you send the first message.
1Waisiraeli wote tunawaona, wameandikwa katika kitabu cha udugu, nao hao walioandikwa wamo katika kitabu cha wafalme wa Waisiraeli; lakini Wayuda walihamishwa kwenda Babeli, kwa kuwa walivunja maagano.[#2 Fal. 24:15-16.]
2Nao wa kwanza waliokaa mijini mwao katika nchi ile, waliyoichukua, iwe yao, walikuwa Waisiraeli waliokuwa watuwatu tu na watambikaji na Walawi na watumishi wa Nyumbani mwa Mungu.[#Yos. 9:23; Ezr. 8:20.]
3Waliokaa mle Yerusalemu wengine walikuwa wana wa Yuda, wengine wana wa Benyamani, wengine wana wa Efuraimu, wengine wa Manase.[#Neh. 11:3-19.]
4Wayuda: Utai, mwana wa Amihudi, mwana wa Omuri, mwana wa Imuri, mwana wa Bani aliye mmoja wao wana wa Peresi, mwana wa Yuda.
5Wengine walikuwa Wasiloni: Asaya aliyekuwa mzaliwa wa kwanza pamoja na wanawe,
6wengine wana wa Zera: Yueli na ndugu zake, wote pamoja ni watu 690.
7Wengine walikuwa wana wa Benyamini: Salu, mwana wa Mesulamu, mwana wa Hodawia, mwana wa Hasenua;
8tena Ibunia, mwana wa Yerohamu, na Ela, mwana wa Uzi, mwana wa Mikiri, na Mesulamu, mwana wa Sefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibunia;
9tena ndugu zao waliofuata kuzaliwa, watu 956. Watu hawa wote walikuwa vichwa vya milango ya baba zao kwao milango yao.
10Wengine walikuwa watambikaji: Yedaya na Yoyaribu na Yakini
11na Azaria, mwana wa Hilkia, mwana wa Mesulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayoti, mwana wa Ahitubu aliyekuwa mkuu Nyumbani mwa Mungu.[#1 Mambo 6:13.]
12Tena Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkia, na Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yazera, mwana wa Mesulamu, mwana wa Mesilemiti, mwana wa Imeri.
13Nao ndugu zao waliokuwa vichwa vya milango ya baba zao, watu 1760, nao ni watu walio mafundi wenye nguvu za kufanya kazi za utumishi wa Nyumbani mwa Mungu.
14Wengine walikuwa Walawi: Semaya, mwana wa Hasubu, mwana wa Azirikamu, mwana wa Hasabia aliyekuwa mmoja wao wana wa Merari.
15Tena Bakibakari, Heresi na Galali na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikiri, mwana wa Asafu.
16Tena Obadia, mwana wa Semaya, mwana wa Galali, mwana wa Yedutuni, na Berekia, mwana wa Asa, mwana wa Elkana aliyekaa katika vijiji vyao Wanetofati.[#1 Mambo 2:54.]
17Wangoja malango: Salumu na Akubu na Talmoni na Ahimani pamoja na ndugu zao; naye Salumu alikuwa kichwa chao,
18naye anashika mpaka leo zamu ya lango la mfalme lililoko upande wa maawioni kwa jua. Hawa ndio walinda malango wa makambi ya wana wa Lawi.
19Naye Salumu, mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, na ndugu zake wa mlango wa baba yake wao Wakora, walikuwa wenye kazi za utumishi wa kuwa wangoja vizingiti vya hilo Hema, nao baba zao walikuwa wakingoja pa kuyaingilia makambi ya Bwana.[#4 Mose 4:18-20.]
20Naye Pinehasi, mwana wa Elazari, alikuwa kale mkuu wao, naye Bwana alikuwa naye.[#4 Mose 25:7-13.]
21Zakari, mwana wa Meselemia, alikuwa mlinda lango la Hema la Mkutano.
22Wao wote waliochaguliwa, wawe walinda vizingiti, walikuwa watu 212; nao walikuwa wameandikwa katika kitabu cha udugu katika vijiji vyao; wao ndio, Dawidi na mtazamaji Samweli waliowaweka kwa kuwategemea.[#1 Sam. 9:9,11.]
23Hao wenyewe na wana wao walikuwa wakisimama penye malango ya Nyumba ya Bwana, ile nyumba ya Hema, na kupokeana zamu.
24Nao hao wangoja malango waliwekwa, waangalie pande zote nne, upepo unakotoka: maawioni kwa jua na machweoni kwa jua, kaskazini na kusini.
25Nao ndugu zao waliokaa vijijini kwao hawakuwa na budi kufika kila siku ya saba, wapokezane nao zamu kwa zamu.
26Nao hawa walinda malango walikuwa na wakuu wanne, hao walikaa hapohapo, kwani walitegemewa hivi. Hizi zilikuwa kazi zao Walawi, tena waliwekwa kuviangalia vyumba na vilimbiko vya Nyumbani mwa Mungu.
27Kwa hiyo walilala usiku pande zote za Nyumba ya Mungu, kwani ilikuwa kazi yao kuiangalia na kuifungua, kila kulipokucha.
28Wengine wao walikuwa wenye kazi za kuviangalia vyombo vya utumishi, kwani huhesabiwa, walipoviingiza Nyumbani, tena walipovitoa.
29Wengine wao waliwekwa kuviangalia vyombo vingine, ndio vyombo vyote vilivyomo Patakatifu, nao unga mwembamba nazo mvinyo nayo mafuta nao ubani nayo manukato.
30Lakini walioyatengeneza mavukizo kwa kuyachanganya hayo manukato walikuwa watambikaji wenyewe.[#2 Mose 30:23-25.]
31Naye Matitia, mmoja wao Walawi, mwana wa kwanza wa Mkora Salumu, akapewa kuziangalia kazi za kutengeneza maandazi ya tambiko, kwani walimtegemea.
32Ndugu zao wengine waliokuwa wana wa Kehati wakapewa kuiangalia mikate, aliyowekewa Bwana, waiweke kila siku ya mapumziko.[#3 Mose 24:5,8.]
33Nao hao ndio waimbaji waliokuwa vichwa vya milango ya baba zao ya Walawi, ndio waliokaa katika vile vyumba, wasiokuwa na kazi nyingine, kwani kazi yao yenyewe iliwataka mchana na usiku.[#1 Mambo 9:14-16.]
34Hawa ndio waliokuwa vichwa vya milango ya baba zao Walawi, maana ni wakuu wa vizazi vyao, nao ndio waliokaa Yerusalemu.
35Mle Gibeoni alikaa Yieli, babake Gibeoni, nalo jina la mkewe lilikuwa Maka.[#1 Mambo 8:29-38.]
36Mwanawe wa kwanza ni Abudoni, tena Suri na Kisi na Baali na Neri na Nadabu
37na Gedori na Ayo na Zakaria na Mikloti.
38Naye Mikloti akamzaa Simeamu. Nao hao walikaa ng'ambo ya ndugu zao kule Yerusalemu kwao ndugu zao.
39Naye Neri akamzaa Kisi, naye Kisi akamzaa Sauli, naye Sauli akamzaa Yonatani, tena Malkisua na Abinadabu na Esibaali.
40Naye mwana wa Yonatani alikuwa Meribu-Baali, naye Meribu-Baali akamzaa Mika.
41Nao wana wa Mika ni Pitoni na Meleki na Tarea na Ahazi.
42Ahazi akamzaa Yara, naye Yara akamzaa Alemeti, tena Azimaweti na Zimuri, naye Zimuri akamzaa Mosa.
43Naye Mosa akamzaa Bina, mwanawe huyo alikuwa Refaya, mwanawe huyo Elasa, mwanawe huyo Aseli.
44Naye Aseli alikuwa mwenye wana sita; nayo haya ndiyo majina yao: Azirikamu, Bokeru na Isimaeli na Saria na Obadia na Hanani; hawa ndio wana wa Aseli.