The chat will start when you send the first message.
1Siku hiyo, watu waliposomewa masikioni pao yaliyoandikwa katika kitabu cha Maonyo, pakaoneka palipoandikwa kwamba: Kale na kale asije Mwamoni wala Mmoabu kuuingia mkutano wa Mungu![#5 Mose 23:3-5.]
2Kwani kale hawakuwajia Waisiraeli na kuwagawia chakula na maji, ila walimpenyezea Bileamu mali, aje kuwaapiza, lakini Mungu alikigeuza hicho kiapizo kuwa mbaraka.[#4 Mose 22:5-6.]
3Kwa hiyo walipoyasikia Maonyo wakawatenga kwao Waisiraeli wote pia waliochanganyika nao.
4Hayo yalipokuwa hayajafanyika bado, mtambikaji Eliasibu alikuwa amewekwa kuviangalia vyumba vya Nyumba ya Mungu. Naye kwa kuwa ndugu yake Tobia
5alimpa chumba kikubwa; ndimo, walimoweka kale vilaji vya tambiko, uvumba na vyombo na mafungu ya kumi: ngano, mvinyo mbichi na mafuta, watu waliyoagizwa kuwapa Walawi, waimbaji na walinda malango, nayo michango ya watambikaji.
6Hayo yote yalipofanyika, mimi nilikuwa simo Yerusalemu, kwani katika mwaka wa thelathini na mbili wa Artasasta, mfalme wa Babeli, nalikwenda kwake mfalme; siku zilipopita, nikamwomba mfalme ruhusa.
7Nilipokuja Yerusalemu nikayatambua hayo mabaya, Eliasibu aliyoyafanya kwa ajili yake Tobia akimpa chumba uani penye Nyumba ya Mungu.
8Nikakasirika sana, nikavitoa vyombo vyote vya nyumbani mwa Tobia mle chumbani, nikavitupa nje,
9nikaagiza, wavitakase hivyo vyumba, kisha nikarudisha humo vyombo vya Nyumba ya Mungu na vilaji vya tambiko na uvumba.[#Neh. 10:39.]
10Nikajulishwa, ya kuwa Walawi hawakupewa mafungu yao yawapasayo; kwa hiyo Walawi na waimbaji waliofanya kazi za Mungu walikuwa wamekimbilia kila mtu shamba lake.
11Ndipo, nilipowagombeza watawalaji na kuwauliza: Mbona Nyumba ya Mungu imeachwa hivyo? Nikawakusanya, nikawaweka tena mahali pao pa utumishi.[#Neh. 10:39.]
12Wayuda wote walipoyaleta tena mafungu ya kumi: ngano na mvinyo mbichi na mafuta na kuyaweka penye vilimbiko,[#4 Mose 18:21.]
13nikaweka watunza vilimbiko, waviangalie hivyo vilimbiko, ndio mtambikaji Selemia na mwandishi Sadoki na Pedaya aliyekuwa Mlawi naye, tena Hanani, mwana wa Zakuri, mwana wa Matania, kuwa msaidiaji wao, kwani hawa waliwaziwa kuwa welekevu, kisha ikawa kazi yao kuwagawia ndugu zao mafungu yao.
14Mungu wangu unikumbukie haya, wala usiyafute matendo ya upole wangu, niliyoitendea Nyumba ya Mungu wangu, kazi zake ziangaliwe vema![#Neh. 5:19; 13:31.]
15Siku hizo nikaona katika nchi ya Yuda, ya kuwa wako wanaokanyaga makamulio siku ya mapumziko, ya kuwa wengine hupeleka machungu ya ngano chanjani kwa kuchukuza punda, wakawatwika hata mvinyo, zabibu, kuyu na mizigo yo yote, wakaipeleka Yerusalemu siku ya mapumziko. Ndipo, nilipowaonya hiyo siku, walipouza vilaji.[#Neh. 10:31; Yer. 17:21-27.]
16Nao Watiro waliokaa huku wakaleta samaki na vingine vyo vyote vya kuuza, wakaviuzia wana wa Yuda namo mle Yerusalemu siku ya mapumziko.
17Nikawagombeza wakuu wa miji ya Yuda na kuwaambia: Hili ni neno baya zaidi, mnalolifanya siku ya mapumziko.
18Je? Baba zenu hawakuyafanya yayo hayo? Hii siyo sababu, Mungu wetu akituletea haya mabaya sisi na mji huu? Kumbe ninyi mwataka kuwapatia Waisiraeli makali yenye moto yaliyo makubwa zaidi, mkiichafua siku ya mapumziko!
19Ndipo, nilipoagiza, milango ifungwe, giza lilipoanza kuingia penye malango ya Yerusalemu siku ya kuiandalia siku ya mapumziko, kisha mikaagiza, isifunguliwa hata siku ifuatayo, ndiyo ya mapumziko, nikachukua vijana wa kwangu, nikawasimamisha malangoni kuangalia, usiingie mzigo wo wote siku ya mapumziko.
20Kwa hiyo wachuuzi na wauzaji wa vitu vyo vyote hawakuwa na budi kulala nje ya Yerusalemu mara moja, hata mara mbili.
21Nikawaonya na kuwaambia: Mbona mnalala mbele ya ukuta? Mkivifanya tena, nitawakamata na kuwafunga. Tangu hapo hawakuja tena siku ya mapumziko.
22Kisha nikawaambia Walawi, wajitakase, kisha waje kiyalinda malango, waitakase siku ya mapumziko. Mungu wangu, haya nayo unikumbukie, kanihurumie kwa upole wako mwingi![#Neh. 13:14.]
23Tena nikaona siku hizo, ya kuwa wako Wayuda waliooa wake wa Waasdodi na wa Waamoni na wa Wamoabu.
24Nao wana wao nusu wakasema Kiasdodi, hawakuweza kusema Kiyuda, ila walisema misemo yao hawa na hawa.
25Nikawagombeza na kuwaapiza na kuwapiga, waume wengine nikawavuta nywele. Kisha nikawaapisha na kumtaja Mungu kwamba: Msiwaoze wana wao wana wenu wa kike, wala msichukue kwao wana wa kike, mwape wana wenu wa kiume au mwaoe wenyewe![#5 Mose 7:3.]
26Je? Siyo haya, Salomo, mfalme wa Isiraeli, aliyoyakosa? Katika mataifa mengi hakuwako mfalme kama yeye, naye alikuwa amependwa na Mungu wake, kwa hiyo Mungu akampa kuwa mfalme wa Waisiraeli wote; lakini naye yeye wanawake wageni wakamkosesha.[#1 Fal. 11:3-8.]
27Tunasikiaje kwenu, ya kuwa mnayafanya hayo mabaya yote yaliyo makubwa, mkiyavunja maagano, tuliyoyafanya na Mungu wetu, kwa kuoa wanawake wageni?
28Mmoja wao wana wa mtambikaji mkuu Yoyada, mwana wa Eliasibu, alikuwa amemwoa binti Mhoroni sanibalati; huyu nikamfukuza, asikae kwangu.[#Neh. 2:19; 11:10.]
29Mungu wangu, wakumbukie hivyo, walivyouchafua utambikaji kwa kuyavunja maagano ya utambikaji na ya Walawi!
30Ndivyo, nilivyowaeua na kuyaondoa mambo yote ya kigeni, nikawasimikia watambikaji na Walawi zamu zao za utumishi wa kila mtu katika kazi yake.
31Nikayatengeneza nayo matoleo ya kuni na ya malimbuko, yafanyike siku zizo hizo zilizowekwa. Mungu wangu, nikumbukie haya, unipatie mema![#Neh. 5:19; 13:14,22.]