The chat will start when you send the first message.
1Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.[#2 Fal 17:4; Isa 30:6]
2BWANA naye ana shutuma juu ya Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.
3Tumboni alimshika ndugu yake kisigino;[#Mwa 25:26]
Na alipokuwa mtu mzima alishindana na Mungu;
4Naam, alishindana na malaika[#Mwa 28:10-22]
Akashinda; alilia, na kumsihi;
Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;
5Naam, BWANA, Mungu wa majeshi;
BWANA ndilo kumbukumbu lake.
6Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.
7Ni mfanya biashara, aliye na mizani ya udanganyifu mkononi mwake; anapenda kudhulumu.
8Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wowote uliokuwa dhambi.
9Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za sikukuu teule.[#Law 23:42-43]
10Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano.
11Katika Gileadi kuna uovu? Nao wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng'ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.[#Amo 4:4]
12Na Yakobo alikimbia mpaka Padan-Aramu,[#Mwa 29:1-20]
Na Israeli alitumika apate mke;
Ili apate mke alichunga kondoo.
13Na kwa nabii BWANA alimtoa Israeli katika Misri,[#Kut 12:50-51]
Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.
14Efraimu amenitia hasira kali sana; kwa sababu hiyo damu yake itaachwa juu yake, na Bwana wake atamrudishia lawama yake.[#Kum 28:37; Dan 11:18]