The chat will start when you send the first message.
1LAKINI kwa khabari ya nyakati na majira, ndugu, hamna haja niwaandikie.
2Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwizi ajavyo usiku.
3Maana wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo niwenye mimba; nao hawataokolewa.
4Bali ninyi, ndugu, hamwi katika giza, siku ile iwapale kama mwizi.
5Maana ninyi nyote wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi hatuwi wa usiku, wala wa giza.
6Bassi tusilale kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
7Maana walalao hulala usiku, na walewao hulewa usiku.
8Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, tukijivika kifuani imani na upendo, na chepeo yetu iwe tumaini la wokofu.
9Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira vake bali tupate wokofu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo,
10aliyekufa kwa ajili vetu, illi tuishi pamoja nae, ikiwa twakesha au ikiwa twalala.
11Bassi, farijianeni mkajengeane, killa mtu mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.
12Lakini, ndugu, tunataka mwajue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu na kuwasimamieni katika Bwana, na kuwaonyeni;
13mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Mwe na amani ninyi kwa ninyi.
14Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.
15Angalieni mtu awae yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
16Furahini siku zote;
17ombeni hila kukonia;
18shukuruni kwa killa jambo; maana haya ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
19Msimzimishe Roho;
20msitweze unabii;
21jaribuni vyote; lishikeni lililo jema;
22jitengeni na ubaya wa killa namna.
23Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
24Yeye ni mwaminifu awaitae, nae atafanya.
25Ndugu, tuombeeni.
26Wasalimuni ndugu kwa husu takatifu.
27Nawaapisha kwa Bwana, wasomewe ndugu wote waraka huu.
28Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi. Amin.