The chat will start when you send the first message.
1LAKINI yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, illakini msimhukumu mawazo yake.
2Mtu mmoja ana imani, anakula vyote, lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.
3Yeye alae asimdharau yeye asiyekula, nae asiyekula asimhukumu yeye alae; kwa maana Mungu amemkubali.
4Wewe u nani unaemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa Bwana wake mwenyewe husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, maana Bwana aweza kumsimamisha.
5Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwingine aona siku zote kuwa sawa sawa. Killa mtu athuhutike katika akili zake mwenyewe.
6Yeye aadhimishae siku, kwa Bwana aiadhimisha; na yeye asiyeadhimisha siku, haiadhimishi kwa Bwana; nae alae, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; nae asiokula, hali kwa Bwana, nae amshukuru Mungu.
7Kwa sababu hapana mtu miongoni mwenu aishiye kwa nafsi yake, wala hapana afae kwa nafsi yake.
8Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Bassi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.
9Maana Kristo alikufa akafufuka akawa hayi tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hayi pia.
10Lakini wewe je! mbona wamhukumu ndugu yako? na wewe je! mbona wamdbarau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.
11Kwa maana imeandikwa,
Kwa uhayi wangu, anena Bwana, magoti yote yatapigwa mbele zangu,
Na ndimi zote zitamkiri Mungu.
12Bassi kama ni hivyo, killa mtu miongoni mwetu atatoa khabari za nafsi yake mbele za Mungu.
13Bassi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali mtoe hukumu hii, ndugu asitiwe kitu cha kumkwaza au cha kumwangusha.
14Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najis asili yake, lakini kwake huyu akionae kitu kuwa najis, kwake huyo kitu kile ni najis.
15Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambae Kristo alikufa kwa ajili yake.
16Bassi, usitajwe vibaya kwa huo wema wenu.
17Maana ufalme wa Muugu si kula na kunywa, bali baki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
18Kwa kuwa yeye amtumikiae Kristo katika mambo haya humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wana Adamu.
19Bassi kama ni hivyo, tufuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana.
20Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Vyote ni safi; bali ni vibaya mtu kula akajikwaza.
21Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno ambalo ndugu yako hukwazwa au kuangushwa au kuwa dhaifu.
22Je! unayo imani? Uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Yu kheri mtu yule asiyejihukumu katika neno lile alikubalilo.
23Lakini aliye na mashaka, kama akila, amehukumiwa, kwa maana hakula kwa imani. Na killa tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.