Warumi 15

Warumi 15

1BASSI imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza nafsi zetu.

2Killa mtu miongoni mwetu ampendeze jirani yake apate wema akajengwe.

3Kwa maana Kristo nae hakujipendeza nafsi yake; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu yalinipata mimi.

4Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa kutufundisha sisi, illi kwa uvumilivu na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.

5Na Mungu mwenye uvumilivu na faraja awajalieni kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa namna ya Yesu Kristo;

6illi kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa liwima wetu Yesu Kristo.

7Kwa hiyo mkaribishane, kama nae Kristo alivyotukaribisha, illi Mungu atukuzwe.

8Bassi nasema, Yesu Kristo amefanyika mkhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithubutishe ahadi walizopewa haha zetu;

9nao Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa,

Kwa sababu hii nitakusifu katika Mataifa,

Na jina lako nitaliimba.

10Na tena anena,

Furahini, Mataifa, pamoja na watu wake.

11Na tena,

Msifuni Bwana, Mataifa wote;

Mpeni sifa watu wote.

12Na tena Isaya anena,

Litakuwa shina la Yesse,

Nae aondokeae kuwatawala Mataifa; ndiye Mataifa watakaemtumaini.

13Bassi Mungu wa tumaini awajazeni furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mataktifu.

14Na mimi mwenyewe, ndugu zangu, nimehakikishwa kwa khahari zenu kama ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana.

15Lakini nimewaandikieni, ndugu zangu, kwa ujasiri zaidi katika sehemu za waraka huu kana kwamba nawakumbusheni, kwa neema ile niliyopewa na Mungu,

16illi niwe kuhani wa Yesu Kristo katika watu wa mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.

17Bassi, nina sababu ya kujisifu katika Kristo Yesu mbele za Mungu.

18Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yanga, mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, kwa nguvu za ishara na maajabu,

19katika nguvu za Roho Mtakatifu; hatta ikawa tangu Yerusalemi, na kando kando yake, hatta Illuriko nimekwisha kuikhubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu,

20kadhalika nikijitahidi kuikhubiri Injili, nisikhubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine,

21bali kama ilivyoandikwa,

Wale wasiokhubiriwa khahari zake wafaona,

Na wale wasiosikia watafahamu.

22Ndio sababu nalizuiwa marra nyingi nisije kwenu.

23Lakini sasa, kwa kuwa sina wasaa tena pande hizi, tena tangu miaka mengi nikiwa na shauku kuja kwenu;

24wakati wo wote nitakaosafiri kwenda Hispania nitakuja kwenu, kwa maana nataraja kuwaona ninyi katika kusafiri kwangu, na kupelekwa mbele nanyi, moyo wangu ushibe kwenu ijapokuwa ni kidogo.

25Na sasa ninakwenda Yerusalemi, nikiwakhudumu watakatifu;

26maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya watakatifu katika Yerusalemi walio maskini.

27Naam, imewapendeza, tena wanawiwa nao. Kwa maana ikiwa mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwakhudumu kwa mambo yao ya mwili.

28Bassi nikiisha kumaliza hazi hii, na kuwatilia muhuri tunda hili, nitapita kwenu na kutoka kwenu nitakwenda Hispania.

29Nami najua ya kuwa nikija kwenu nitakuja kwa utimilifu wa haraka ya Injili ya Kristo.

30Nakusihini, ndugu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami kwa maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu,

31niokolewe nao waasio katika Yahudi, na tena khuduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemi ipate kibali kwa watakatifu,

32nipate kufika kwenu kwa furaha, kama Mungu akipenda, nikapate kupumzika pamoja nanyi.

33Mungu wa amani awe pamoja nanyi nyote. Amin.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania