Zaburi 125

Zaburi 125

Usalama wa watu wa Mungu

1Wanaomtegemea Mwenyezi-Mungu, wako kama mlima Siyoni,

ambao hautikisiki bali wabaki imara daima.

2Kama Yerusalemu inavyozungukwa na milima,

ndivyo Mwenyezi-Mungu awazungukavyo watu wake,

tangu sasa na hata milele.

3Waovu hawataendelea kutawala nchi ya waadilifu;

wasije waadilifu nao wakafanya maovu.

4Ee Mwenyezi-Mungu, uwe mwema kwa watu wema,

kwa wale wanaozitii amri zako.

5Lakini wanaogeuka na kufuata njia zao mbaya

uwakumbe pamoja na watenda maovu.

Amani iwe na Israeli!

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania