The chat will start when you send the first message.
1Mwenyezi-Mungu asipoijenga nyumba,
waijengao wanajisumbua bure.
Mwenyezi-Mungu asipoulinda mji,
waulindao wanakesha bure.
2Mnajisumbua bure kuamka mapema asubuhi
na kuchelewa kwenda kupumzika jioni,
mjipatie chakula kwa jasho lenu.
Mungu huwaruzuku walio wake hata walalapo.
3Watoto ni riziki kutoka kwa Mwenyezi-Mungu;
watoto ni tuzo lake kwetu sisi.
4Watoto waliozaliwa wazazi wakiwa bado vijana,
ni kama mishale mikononi mwa askari.
5Heri mtu aliye na mishale hiyo kwa wingi.
Hatashindwa atakapokabiliana na adui mahakamani.