1 Mambo ya Nyakati 8

1 Mambo ya Nyakati 8

Wazawa wa Benyamini

1Benyamini alikuwa na wana watano: Bela, mzaliwa wake wa kwanza, Ashbeli wa pili, Ahara wa tatu,[#8:1 Huyu ndiye aliyekuwa mtoto wa mwisho wa Yakobo. Mara baada ya kuzaliwa, mama yake yaani Raheli, alifariki (rejea Mwa 35:16-20). Benyamini alipendwa na Yakobo (rejea Mwa 42:4,38; 44:18-34). Alikuwa nduguye Yosefu (rejea Mwa 30:22-24,25; 35:24; 42:13—45:15). Mwandishi wa simulizi la 1 Mambo ya Nyakati analipa kabila la Benyamini nafasi maalumu labda kwa sababu mfalme wa kwanza kabisa kutawala Waisraeli, Shauli, alitoka katika kabila hilo. Zaidi ya hayo kabila hilo la Benyamini lilikuwa mojawapo ya makabila yaliyosaidia kujenga upya Yerusalemu chini ya uongozi wa Nehemia (Neh 11:7-9) wakati Waisraeli waliporudi kutoka uhamishoni Babuloni. Tena, mji wa Yerusalemu ulikuwa katika eneo ambalo lilikuwa la kabila hilo.]

2Noha wa nne na Rafa wa tano.[#8:2-7 Rejea orodha tofautitofauti katika 7:2-12; Mwa 46:21; Hes 26:38-41.]

3Bela naye alikuwa na wana: Adari, Gera, Abihudi,

4Abishua, Naamani, Ahoa,

5Gera, Shufamu na Huramu.

6Hawa ndio wazawa wa Ehudi. Hawa walikuwa viongozi wa jamaa za wale waliokuwa wakiishi Geba, lakini wakachukuliwa mateka uhamishoni Manahathi;

7Naamani, Ahiya na Gera. Gera, baba yake Uza na Ahihudi, ndiye aliyewaongoza kuchukua hatua hiyo.

8Shaharaimu aliwapa talaka wake zake wawili, Hushimu na Baara na baadaye alipata watoto wa kiume nchini Moabu.

9Alimwoa Hodeshi, naye akamzalia wana saba: Yoabu, Sibia, Mesha, Malkamu,

10Yeuzi, Sakia, na Mirma. Hawa wanawe wote walikuja kuwa wakuu wa koo.

11Shaharaimu na mkewe Hushimu alipata wana wengine wawili: Abitubu na Elpaali.

12Wana wa Elpaali walikuwa watatu: Eberi, Mishamu na Shemedi ambaye aliijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji kandokando yake.

Wabenyamini walioishi Gathi na Aiyaloni

13Beria na Shema walikuwa miongoni mwa jamaa ambazo zilikuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na kuwafukuza wenyeji wa Gathi.

14Nao Ahio, Shashaki, Yeremothi,

15Zebadia, Aradi, Ederi,

16Mikaeli, Ishpa na Yoha ni wazawa wengine wa Beria.

17Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi,

18Ishnerai, Izlia na Yobabu walikuwa wazawa wa Epaali.

19Yakimu, Zikri, Zabdi,

20Elienai, Zilethai, Elieli,

21Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wazawa wa Shimei.

22Ishpani, Eberi, Elieli,

23Abdoni, Zikri, Hanani,

24Hanania, Elamu, Anthothiya,

25Ifdeya na Penueli walikuwa wazawa wa Shashaki.

26Shamsherai, Sheharia, Athalia,

27Yaareshia, Elia na Zikri walikuwa baadhi ya wazawa wa Yerohamu.

28Hao ndio waliokuwa wakuu wa koo zao kulingana na vizazi vyao. Walikuwa wakuu na waliishi Yerusalemu.

Wabenyamini walioishi Gibeoni na Yerusalemu

29Yeieli, alikuwa mwanzilishi wa mji wa Gibeoni. Mkewe alikuwa Maaka.

30Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Abdoni. Wanawe wengine ni Zuri, Kishi, Baali, Nadabu,

31Gedori, Ahio, Zekeri,

32na Miklothi baba yake Shimea. Hawa pia waliishi Yerusalemu karibu na watu wengine wa ukoo wao.

Ukoo wa mfalme Shauli

33Neri alimzaa Kishi, Kishi akamzaa Shauli. Shauli alikuwa na wana wanne: Yonathani, Malki-shua, Abinadabu na Eshbaali.[#8:33 Labda hili ndilo jina lake la asili na maana yake ni “mtu wa Baali”, lakini anaitwa pia “Ishboshethi” (2Sam 2:8), maana yake “mtu wa aibu”.]

34Yonathani alimzaa Merib-baali, na Merib-baali akamzaa Mika.[#8:34 Jina hili ambalo linatumiwa badala ya jina “Mefiboshethi” (2Sam 4:4) lilikuwa limeandikwa awali kama “Merib-baali” maana yake “Shujaa wa Baali” ambalo lilibadilishwa baadaye kuwa “Merib-baali” maana yake: “Mpinzani wa Baali”. Maana ya jina “Mefiboshethi” ni “kutoka mdomo wa aibu”.]

35Mika alikuwa na wana wanne: Pithoni, Meleki, Terea na Ahazi.

36Ahazi alimzaa Yehoada. Naye Yehoada aliwazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri. Zimri alimzaa Mosa.

37Mosa alimzaa Binea, aliyemzaa Rafa, aliyemzaa Eleasa, naye Eleasa akamzaa Aseli.

38Wana wa Aseli walikuwa sita: majina yao ni Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Wote hawa walikuwa wana wa Aseli.

39Nao wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa watatu. Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti.

40Wana wa Ulamu walikuwa watu mashujaa sana wa vita, na wapiga upinde hodari. Alikuwa na wana na wajukuu wengi, jumla150. Hao wote waliotajwa hapo juu walikuwa wa ukoo wa Benyamini.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993 The Bible Society of Kenya 1993
Published by: Bible Society of Tanzania