Zaburi 100

Zaburi 100

Wimbo wa sifa

1Mshangilieni Mwenyezi-Mungu, enyi nchi zote!

2Mwabuduni Mwenyezi-Mungu kwa furaha,

nendeni kwake mkiimba kwa shangwe!

3Jueni kwamba Mwenyezi-Mungu ni Mungu.

Yeye ndiye aliyetuumba, nasi ni mali yake;

sisi ni watu wake, ni kondoo wa malisho yake.

4Pitieni milango ya hekalu lake kwa shukrani,

ingieni katika nyua zake kwa sifa.

Mshukuruni na kulisifu jina lake.

5Mwenyezi-Mungu ni mwema;

fadhili zake zadumu milele,

na uaminifu wake katika vizazi vyote.

Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993 The Bible Society of Kenya 1993
Published by: Bible Society of Tanzania