1 Nyakati 25

1 Nyakati 25

Waimbaji

1Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani, na wana wa Yeduthuni kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hiyo:

2Kutoka kwa wana wa Asafu walikuwa:

3Wana wa Yeduthuni walikuwa sita:

4Wana wa Hemani walikuwa:

6Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu la Bwana wakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme.

7Pamoja na ndugu zao, wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwa Bwana . Idadi yao walikuwa mia mbili na themanini na nane (288).

8Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura.

9Kura ya kwanza, ambayo ilikuwa kwa ajili ya Asafu, ilimwangukia Yusufu, wanawe na jamaa zake, 12;

Ya pili ikamwangukia Gedalia, yeye na wanawe pamoja na jamaa zake, 12;

10Ya tatu ikamwangukia Zakuri, wanawe na jamaa zake, 12;

11ya nne ikamwangukia Isri, wanawe na jamaa zake, 12;[#25:11 au Seri]

12ya tano ikamwangukia Nethania, wanawe na jamaa zake, 12;

13ya sita ikamwangukia Bukia, wanawe na jamaa zake, 12;

14ya saba ikamwangukia Yesarela, wanawe na jamaa zake, 12;[#25:14 au Asarela]

15ya nane ikamwangukia Yeshaya, wanawe na jamaa zake, 12;

16ya tisa ikamwangukia Matania, wanawe na jamaa zake, 12;

17ya kumi ikamwangukia Shimei, wanawe na jamaa zake, 12;

18ya kumi na moja ikamwangukia Azareli, wanawe na jamaa zake, 12;[#25:18 au Uzieli]

19ya kumi na mbili ikamwangukia Hashabia, wanawe na jamaa zake, 12;

20ya kumi na tatu ikamwangukia Shubaeli, wanawe na jamaa zake, 12;

21ya kumi na nne ikamwangukia Matithia, wanawe na jamaa zake, 12;

22ya kumi na tano ikamwangukia Yeremothi, wanawe na jamaa zake, 12;

23Ya kumi na sita ikamwangukia Hanania, wanawe na jamaa zake, 12;

24ya kumi na saba ikamwangukia Yoshbekasha, wanawe na jamaa zake, 12;

25ya kumi na nane ikamwangukia Hanani, wanawe na jamaa zake, 12;

26ya kumi na tisa ikamwangukia Malothi, wanawe na jamaa zake, 12;

27ya ishirini ikamwangukia Eliatha, wanawe na jamaa zake, 12;

28ya ishirini na moja ikamwangukia Hothiri, wanawe na jamaa zake, 12;

29ya ishirini na mbili ikamwangukia Gidalti, wanawe na jamaa zake, 12;

30ya ishirini na tatu ikamwangukia Mahaziothi, wanawe na jamaa zake, 12;

31ya ishirini na nne ikamwangukia Romamti-Ezeri, wanawe na jamaa zake, 12.

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.