The chat will start when you send the first message.
1Hiramu mfalme wa Tiro aliposikia kuwa Sulemani amepakwa mafuta awe mfalme mahali pa Daudi baba yake, akatuma wajumbe kwa Sulemani, kwa sababu Hiramu siku zote alikuwa na uhusiano mzuri wa kirafiki na Daudi.
2Sulemani akapeleka ujumbe huu kwa Hiramu:
7Hiramu aliposikia ujumbe wa Sulemani, akafurahishwa sana akasema, “Ahimidiwe Bwana leo, kwa kuwa amempa Daudi mwana mwenye hekima ya kutawala taifa hili kubwa.”
8Hivyo Hiramu akapeleka ujumbe kwa Sulemani:
10Kwa njia hii Hiramu akampa Sulemani miti yote ya mierezi na magogo ya misunobari kama alivyohitaji,
11naye Sulemani akampa Hiramu kori elfu ishirini za ngano kama chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, pamoja na mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa bathi elfu ishirini. Sulemani aliendelea kumfanyia Hiramu hivyo mwaka baada ya mwaka.[#5:11 Kori 20,000 ni sawa na madebe 240,000.; #5:11 Bathi 20,000 ni sawa na madebe 200.]
12Bwana akampa Sulemani hekima, kama alivyomwahidi. Palikuwa na uhusiano wa amani kati ya Hiramu na Sulemani, na wote wawili wakafanya mkataba.
13Mfalme Sulemani akakusanya wafanyakazi elfu thelathini kutoka Israeli yote.
14Akawapeleka Lebanoni kwa zamu za watu elfu kumi kila mwezi. Hivyo walikaa Lebanoni kwa mwezi mmoja, na miezi miwili wakakaa nyumbani. Adoniramu ndiye alikuwa kiongozi wa shokoa.
15Sulemani alikuwa na wachukuzi wa mizigo elfu sabini, na wachonga mawe elfu themanini huko vilimani,
16pamoja na wasimamizi elfu tatu mia tatu ambao walisimamia mradi huo na kuwaelekeza wafanyakazi.
17Kwa amri ya mfalme, walitoa mawe makubwa na bora kwenye machimbo ya mawe kwa kujengea msingi wa mawe yaliyochongwa kwa ajili ya Hekalu.
18Mafundi wa Sulemani, wa Hiramu na watu wa Gebali walikata na kuandaa mbao na mawe kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu.[#5:18 yaani Bubilo]