2 Nyakati 17

2 Nyakati 17

Yehoshafati mfalme wa Yuda

1Yehoshafati mwanawe akawa mfalme baada yake na akajiimarisha dhidi ya Israeli.

2Akaweka jeshi katika miji yote ya Yuda yenye ngome, na kuweka askari walinzi katika Yuda na katika miji ya Efraimu ambayo baba yake Asa alikuwa ameiteka.

3Bwana Mungu alikuwa na Yehoshafati kwa sababu katika miaka yake ya mwanzoni alienenda katika njia za Daudi baba yake. Hakutafuta Mabaali

4bali alimtafuta Mungu wa baba yake na kuzifuata amri zake badala ya kufuata desturi za Waisraeli.

5Kwa hiyo Bwana akauimarisha ufalme chini ya uongozi wake, nao Yuda wote wakamletea Yehoshafati zawadi, hivyo akawa na utajiri mwingi na heshima.

6Moyo wake ukawa hodari katika njia za Bwana na zaidi ya yote, akaondoa mahali pa juu pa kuabudia na nguzo za Maashera katika Yuda.

7Katika mwaka wa tatu wa utawala wake Yehoshafati, alituma maafisa wake ambao ni Ben-Haili, Obadia, Zekaria, Nethaneli na Mikaya ili kufundisha katika miji ya Yuda.

8Pamoja nao walikuwa na Walawi kadhaa: Shemaya, Nethania, Zebadia, Asaheli, Shemiramothi, Yehonathani, Adoniya, Tobia, Tob-Adonia; na pamoja nao makuhani Elishama na Yehoramu.

9Wakafundisha Yuda yote, wakiwa wamechukua Kitabu cha Sheria ya Bwana ; wakazunguka miji yote ya Yuda na kufundisha watu.

10Kicho cha Bwana kikawa juu ya falme zote za nchi zilizozunguka Yuda, hivyo hawakufanya vita na Yehoshafati.

11Baadhi ya Wafilisti wakamletea Yehoshafati zawadi na fedha kama ushuru, nao Waarabu wakamletea mifugo: kondoo dume elfu saba na mia saba, na mbuzi elfu saba na mia saba.

12Yehoshafati akaendelea kupata nguvu zaidi na zaidi, akajenga ngome na miji ya hazina katika Yuda,

13na akawa na vifaa vingi katika miji ya Yuda. Pia aliweka wapiganaji wenye uzoefu huko Yerusalemu.

14Wakaandikishwa katika jamaa zao kama ifuatavyo:

Kutoka Yuda, majemadari wa vikosi vya elfu:

17Kutoka Benyamini:

19Hawa ndio wapiganaji waliomtumikia mfalme, mbali na ambao mfalme aliwaweka katika miji yenye ngome katika Yuda yote.

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.