The chat will start when you send the first message.
1Ikawa baada ya jambo hili, Wamoabu na Waamoni, pamoja na baadhi ya Wameuni wakaja ili wapigane vita na Yehoshafati.
2Watu fulani wakaja wakamwambia Yehoshafati, “Jeshi kubwa linakuja dhidi yako kutoka Shamu tokea ngʼambo ile nyingine ya Bahari. Tayari liko Hasason-Tamari” (yaani En-Gedi).[#20:2 yaani Bahari ya Chumvi.]
3Yehoshafati akaogopa, akaamua kumtafuta Bwana , na akatangaza kwa Yuda wote kufunga.
4Watu wa Yuda wakakusanyika pamoja ili kutafuta msaada kutoka kwa Bwana . Wakaja kutoka kila mji wa Yuda ili kumtafuta.
5Kisha Yehoshafati akasimama katika kusanyiko la Yuda na Yerusalemu katika Hekalu la Bwana , mbele ya ua mpya,
6akasema:
13Wanaume wote wa Yuda pamoja na wake zao, watoto wao na wadogo wao wakasimama pale mbele za Bwana .
14Ndipo Roho wa Bwana akaja juu ya mtu mmoja jina lake Yahazieli mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, Mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, Mlawi mzao wa Asafu alipokuwa amesimama katika kusanyiko.
15Akasema: “Sikilizeni, enyi Yuda wote nanyi nyote mnaoishi Yerusalemu, nawe Mfalme Yehoshafati! Hili ndilo asemalo Bwana kwenu, ‘Msiogope wala msifadhaike kwa sababu ya jeshi hili kubwa. Kwa maana vita hivi si vyenu, bali ni vya Mungu.
16Kesho shukeni kukabiliana nao. Watakwea kwa kupandia Genge la Sisi, nanyi mtawakuta mwisho wa bonde, kabla ya Jangwa la Yerueli.
17Hamtahitaji kupigana vita hivi. Kaeni kwenye nafasi zenu, simameni imara na mkaone wokovu Bwana atakaowapatia, enyi Yuda na Yerusalemu. Msiogope, wala msifadhaike. Kesho tokeni mwende mkawakabili, naye Bwana atakuwa pamoja nanyi.’ ”
18Yehoshafati akasujudu, uso wake ukigusa chini, nao watu wote wa Yuda na Yerusalemu wakasujudu na kuabudu mbele za Bwana .
19Ndipo baadhi ya Walawi kutoka kwa Wakohathi na kwa wana wa Kora wakasimama na kumsifu Bwana , Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana.
20Asubuhi na mapema wakaondoka kuelekea Jangwa la Tekoa. Walipoanza safari, Yehoshafati akasimama akasema, “Nisikilizeni, enyi Yuda, na watu wa Yerusalemu! Mwaminini Bwana Mungu wenu, hivyo mtathibitika, wasadikini manabii wake nanyi mtafanikiwa.”
21Alipomaliza kushauriana na watu, Yehoshafati akawaweka watu wa kumwimbia Bwana na kumsifu katika utukufu wa utakatifu wake walipokuwa wametangulia mbele ya jeshi, wakisema:
“Mshukuruni Bwana
kwa kuwa fadhili zake zadumu milele.”
22Walipoanza kuimba na kusifu, Bwana akaweka waviziaji dhidi ya watu wa Amoni, Moabu na wale wa Mlima Seiri waliokuwa wamekuja kuishambulia Yuda, nao wakashindwa.
23Watu wa Amoni na Moabu wakawainukia watu wa Mlima Seiri ili kuwaua na kuwaangamiza kabisa. Baada ya kumaliza kuwachinja watu wa Seiri, wakaangamizana wao kwa wao.
24Yuda walipofika katika mnara wa ulinzi wa jangwani, wakaliangalia lile jeshi kubwa, wakaona ni maiti tupu zimetapakaa ardhini, wala hakuna yeyote aliyenusurika.
25Hivyo Yehoshafati na watu wake wakaenda kujitwalia nyara kutoka kwao, nao wakakuta humo wingi wa mifugo, mali, mavazi na vitu vya thamani, ambavyo vilikuwa vingi zaidi ya vile walivyoweza kuchukua. Wakakusanya nyara kwa siku tatu kwa sababu zilikuwa nyingi mno.
26Siku ya nne wakakusanyika katika Bonde la Beraka, mahali walikomtukuza Bwana . Ndiyo sababu linaitwa Bonde la Beraka hadi leo.[#20:26 Bonde la Beraka maana yake Bonde la Kusifu.]
27Kisha wanaume wote wa Yuda na Yerusalemu, wakiongozwa na Yehoshafati, wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha, kwa kuwa Bwana alikuwa amewasababisha wafurahi juu ya adui zao.
28Wakaingia Yerusalemu na kwenda hekaluni mwa Bwana wakiwa na vinubi, zeze na tarumbeta.
29Hofu ya Mungu ikazipata falme zote za nchi waliposikia jinsi Bwana alivyokuwa amepigana dhidi ya adui za Israeli.
30Ufalme wa Yehoshafati ukawa na amani, kwa kuwa Mungu wake alikuwa amempa amani pande zote.
31Hivyo Yehoshafati akatawala Yuda. Alikuwa na umri wa miaka thelathini na tano alipoanza kutawala, akatawala katika Yerusalemu kwa miaka ishirini na tano. Mama yake aliitwa Azuba binti Shilhi.
32Alienenda katika njia za Asa baba yake wala hakuenda kinyume chake. Alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana .
33Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa, na watu wakawa bado hawajaelekeza mioyo yao kwa Mungu wa baba zao.
34Matukio mengine ya utawala wa Yehoshafati, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Yehu mwana wa Hanani, ambazo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli.
35Hatimaye Yehoshafati mfalme wa Yuda akafanya mapatano na Ahazia mfalme wa Israeli, ambaye alifanya maovu sana.
36Akaungana naye kutengeneza meli nyingi za kwenda Tarshishi, nazo zilitengenezwa huko Esion-Geberi.[#20:36 au: za biashara (taz. 1Fal 10:22; 22:48; 2Nya 9:21; Isa 2:16; 60:9).]
37Ndipo Eliezeri mwana wa Dodavahu wa Maresha akatoa unabii dhidi ya Yehoshafati, akasema, “Kwa kuwa umeungana na Ahazia, Bwana ataangamiza vile mlivyotengeneza.” Zile meli zikavunjika na hazikuweza kungʼoa nanga ili kwenda Tarshishi.