2 Yohana 1

2 Yohana 1

Salamu

Kweli na upendo

4Imenipa furaha kuu kuona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile Baba alivyotuagiza.

5Sasa, mama mteule mpendwa, si kwamba ninakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo. Tupendane kila mmoja na mwenzake.

6Hili ndilo pendo: kwamba tuenende kwa kuzitii amri zake. Hii ndiyo amri yake kama vile mlivyosikia tangu mwanzo, kwamba mwenende katika upendo.

7Wadanganyifu wengi, wasiokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili, wametawanyika ulimwenguni. Mtu kama huyo ni mdanganyifu na mpinga Kristo.

8Jihadharini msije mkapoteza kile mlichokitenda, bali mpate kupewa thawabu kamilifu.

9Mtu yeyote asiyedumu katika mafundisho ya Kristo bali ameyaacha, yeye hana Mungu. Yeyote anayedumu katika mafundisho ana Baba na Mwana pia.

10Msimpokee mtu yeyote anayewajia ambaye hawaletei mafundisho haya, wala msimkaribishe nyumbani mwenu.

11Yeyote amkaribishaye mtu kama huyo anashiriki katika matendo yake maovu.

Salamu za mwisho

12Ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sitaki kutumia karatasi na wino. Badala yake, nataraji kuja kwenu na kuongea nanyi ana kwa ana, ili furaha yetu ipate kuwa timilifu.

13Watoto wa dada yako mteule wanakusalimu. Amen.

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.