Yoshua 19

Yoshua 19

Mgawo kwa Simeoni

Beer-Sheba (au Sheba), Molada,

3Hasar-Shuali, Bala, Esemu,

4Eltoladi, Bethuli, Horma,

5Siklagi, Beth-Markabothi, Hasar-Susa,

6Beth-Lebaothi na Sharuheni; hii ilikuwa miji kumi na tatu pamoja na vijiji vyake.

7Pia Aini, Rimoni, Etheri, na Ashani; hii ilikuwa miji minne na vijiji vyake,

8pamoja na vijiji vyote vinavyoizunguka miji hii hadi Baalath-Beeri (ambayo ndiyo Rama iliyo katika Negebu).

Mgawo kwa Zabuloni

Mpaka wa urithi wao uliendelea hadi Saridi.

11Kuelekea upande wa magharibi ukafika Marala, ukagusa Dabeshethi, na kuendelea hadi kwenye bonde karibu na Yokneamu.

12Ukageuka mashariki, kuanzia Saridi kuelekea mawio ya jua hadi kwenye nchi ya Kisiloth-Tabori, na kwenda hadi Daberathi, kupanda Yafia.

13Kisha ukaendelea mashariki hadi Gath-Heferi na kufika Eth-Kasini, ukatokea Rimoni na kugeuka kuelekea Nea.

14Huko mpaka ukazungukia upande wa kaskazini hadi Hanathoni na kuishia katika Bonde la Ifta-Eli.

15Miji mingine iliyojumuishwa ni Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na mbili pamoja na vijiji vyake.

Mgawo kwa Isakari

Yezreeli, Kesulothi, Shunemu,

19Hafaraimu, Shioni, Anaharathi,

20Rabithi, Kishioni, Ebesi,

21Remethi, En-Ganimu, En-Hada na Beth-Pasesi.

22Mpaka ule ukagusa Tabori, Shahasuma na Beth-Shemeshi, na ukaishia kwenye Yordani.

Ilikuwa miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.

Mgawo kwa Asheri

Helkathi, Hali, Beteni, Akshafu,

26Alameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi.

27Tena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto.

28Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu.

29Mpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika eneo la Akzibu,

30Uma, Afeki na Rehobu.

Ilikuwa miji ishirini na mbili, pamoja na vijiji vyake.

Mgawo kwa Naftali

33Mpaka wao uliendelea kutoka Helefi na kwenye mwaloni ulio Saananimu, ukipitia Adami-Nekebu na Yabineeli hadi Lakumu, na kuishia katika Mto Yordani.

34Mpaka ukaendelea magharibi kupitia Aznoth-Tabori na kutokea Hukoki. Ukagusa Zabuloni upande wa kusini, Asheri upande wa magharibi, na Yordani upande wa mashariki.

35Miji yenye ngome ilikuwa Sidimu, Seri, Hamathi, Rakathi, Kinerethi,

36Adama, Rama, Hazori,

37Kedeshi, Edrei, na En-Hasori,

38Ironi, Migdal-Eli, Horemu, Beth-Anathi na Beth-Shemeshi.

Kulikuwa na miji kumi na tisa na vijiji vyake.

Mgawo kwa Dani

Sora, Eshtaoli, Iri-Shemeshi,

42Shaalabini, Aiyaloni, Ithla,

43Eloni, Timna, Ekroni,

44Elteke, Gibethoni, Baalathi,

45Yehudi, Bene-Beraki, Gath-Rimoni,

46Me-Yarkoni na Rakoni, pamoja na eneo linalotazamana na Yafa.

Mgawo kwa Yoshua

49Walipomaliza kuigawa nchi kulingana na sehemu zilizowaangukia, Waisraeli walimpa Yoshua mwana wa Nuni urithi kati yao,

50kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru. Walimpa mji alioutaka, ambao ni Timnath-Sera ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu. Naye akajenga mji, akakaa huko.[#19:50 Unajulikana pia kama Timnath-Heresi (taz. Yos 24:30; Amu 2:9).]

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.