Malaki 4

Malaki 4

Siku ya Bwana

1“Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na watenda maovu watakuwa mabua makavu, na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asema Bwana wa majeshi. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao.

2Bali ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini.

3Kisha ninyi mtawakanyaga waovu, nao watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu siku ile nitakayofanya mambo haya,” asema Bwana wa majeshi.

4“Kumbukeni sheria ya mtumishi wangu Musa, amri na sheria nilizompa huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote.

5“Tazama, nitawapelekea nabii Eliya kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kutisha ya Bwana .

6Ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, la sivyo nitakuja na kuipiga nchi kwa laana.”

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.