The chat will start when you send the first message.
1Baada ya hiyo tauni, Bwana akamwambia Musa na Eleazari mwana wa kuhani Haruni,
2“Hesabu jumuiya yote ya Waisraeli kufuatana na jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, wanaoweza kutumika katika jeshi la Israeli.”
3Hivyo Musa na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ngʼambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema,
4“Hesabuni wanaume wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kama Bwana alivyomwagiza Musa.”
5Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa:
12Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa:
15Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa:
20Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa:
23Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa:
26Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa:
35Hawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao:
38Wazao wa Benyamini kwa koo zao walikuwa:
42Hawa walikuwa wazao wa Dani kwa koo zao:
44Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa:
48Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa:
52Bwana akamwambia Musa,
53“Watagawiwa nchi kama urithi kulingana na hesabu ya majina.
54Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa.
55Hakikisha kuwa nchi inagawanywa kwa kura. Kile kitakachorithiwa na kila kikundi kitakuwa kwa kulingana na majina ya kabila la babu yao.
56Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.”
57Hawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao:
58Hizi pia zilikuwa koo za Walawi:
63Hawa ndio walioorodheshwa na Musa na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani, ngʼambo ya Yeriko.
64Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa miongoni mwa wale waliohesabiwa na Musa na kuhani Haruni wakati waliwahesabu Waisraeli katika Jangwa la Sinai.
65Kwa maana Bwana alikuwa amewaambia hao Waisraeli hakika wangekufa huko jangwani, wala hakuna mmoja wao aliyeachwa, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni.