Hesabu 7

Hesabu 7

Sadaka za kuweka wakfu Maskani ya Bwana

1Musa alipomaliza kuisimamisha Maskani, aliipaka mafuta na kuiweka wakfu pamoja na samani zake zote. Pia alitia madhabahu mafuta na kuiweka wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote.

2Ndipo viongozi wa Israeli, wale wakuu wa jamaa waliokuwa viongozi wa kabila wasimamizi wa wale waliohesabiwa, wakatoa sadaka.

3Walizileta kama matoleo yao mbele za Bwana : magari sita ya kukokotwa yaliyofunikwa, pamoja na maksai kumi na wawili; yaani maksai mmoja kutoka kwa kila kiongozi, na gari moja la kukokotwa kutoka kwa kila viongozi wawili. Haya waliyaleta mbele ya Maskani.

4Bwana akamwambia Musa,

5“Vikubali vitu hivi kutoka kwao, ili viweze kutumika katika kazi kwenye Hema la Kukutania. Wapatie Walawi kama kazi ya kila mtu itakavyohitaji.”

6Hivyo Musa akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai, na kuwapa Walawi.

7Aliwapa Wagershoni magari mawili ya kukokotwa na maksai wanne, kama walivyohitaji kwa kazi yao,

8na pia aliwapa Wamerari magari manne ya kukokotwa na maksai wanane, kama kazi yao ilivyohitaji. Wote walikuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Haruni.

9Lakini Musa hakuwapa Wakohathi chochote kati ya hivyo, kwa sababu walitakiwa kubeba vitu vitakatifu mabegani mwao, vile walikuwa wanawajibika.

10Madhabahu yalipopakwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu.

11Kwa maana Bwana alikuwa amemwambia Musa, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.”

13Sadaka yake ilikuwa:

19Sadaka aliyoleta ilikuwa:

25Sadaka aliyoleta ilikuwa:

31Sadaka aliyoleta ilikuwa:

37Sadaka aliyoleta ilikuwa:

43Sadaka aliyoleta ilikuwa:

49Sadaka aliyoleta ilikuwa:

55Sadaka aliyoleta ilikuwa:

61Sadaka aliyoleta ilikuwa:

67Sadaka aliyoleta ilikuwa:

73Sadaka aliyoleta ilikuwa:

79Sadaka aliyoleta ilikuwa:

84Hizi ndizo sadaka zilizotolewa na viongozi wa Israeli madhabahu yalipowekwa wakfu, wakati yalipakwa mafuta:

89Musa alipoingia kwenye Hema la Kukutania kuzungumza na Bwana , alisikia sauti ikisema naye kutoka kati ya wale makerubi wawili waliokuwa juu ya kile kiti cha rehema, juu ya Sanduku la Ushuhuda. Musa akazungumza na Bwana .

Neno: Biblia Takatifu™ Neno™ Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote. Kiswahili Contemporary Version™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. Used with permission. All rights reserved worldwide.
Published by: Biblica, Inc.