The chat will start when you send the first message.
1Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako,
ikiwa umeshikana mikono kwa kuweka ahadi
kwa ajili ya mwingine,
2kama umetegwa na ulichosema,
umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,
3basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru,
kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako:
Nenda ukajinyenyekeshe kwake;
msihi jirani yako!
4Usiruhusu usingizi machoni pako,
usiruhusu kope zako zisinzie.
5Jiweke huru, kama paa kutoka mkononi mwa mwindaji,
kama ndege kutoka mtego wa mwindaji.
6Ewe mvivu, mwendee mchwa;
zitafakari njia zake ukapate hekima!
7Kwa maana yeye hana msimamizi,
wala mwangalizi, au mtawala,
8lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi
na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.
9Ewe mvivu, utalala hata lini?
Utaamka lini kutoka usingizi wako?
10Kulala kidogo, kusinzia kidogo,
kukunja mikono kidogo upate kupumzika:
11umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi,
na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.
12Mtu mbaya sana na mlaghai,
ambaye huzungukazunguka
13ambaye anakonyeza kwa jicho lake,
anayetoa ishara kwa miguu yake
na kuashiria kwa vidole vyake,
14ambaye hupanga ubaya
daima huchochea fitina.
15Kwa hiyo maafa yatamkumba ghafula;
ataangamizwa mara moja, pasipo msaada.
16Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana ,
20Mwanangu, zishike amri za baba yako,
wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
21Yafunge katika moyo wako daima,
yakaze kuizunguka shingo yako.
22Unapotembea, yatakuongoza;
unapolala, yatakulinda;
unapoamka, yatazungumza nawe.
23Kwa maana amri hii ni taa,
mafundisho haya ni mwanga,
na maonyo ya nidhamu
ni njia ya uzima,
24yakikulinda na mwanamke aliyepotoka,
kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka.
25Moyo wako usitamani uzuri wake,
wala macho yake yasikuteke,
26kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini,
hata ukose kipande cha mkate,
naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa.
27Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake
bila nguo zake kuungua?
28Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto
bila miguu yake kuungua?
29Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine;
hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa.
30Watu hawamdharau mwizi akiiba
ili kukidhi njaa yake akiwa na njaa.
31Lakini akikamatwa, lazima alipe mara saba,
ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake.
32Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.
33Mapigo na aibu ni fungu lake
na aibu yake haitafutika kamwe;
34kwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume,
naye hataonesha huruma alipizapo kisasi.
35Hatakubali fidia yoyote;
atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani.