The chat will start when you send the first message.
1Katika dhiki yangu namwita Mwenyezi Mungu,
naye hunijibu.
2Ee Mwenyezi Mungu, uniokoe kutoka midomo ya uongo
na ndimi za udanganyifu.
3Atakufanyia nini,
au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?
4Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa,
kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.
5Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki,
kwamba naishi katikati ya mahema ya Kedari!
6Nimeishi muda mrefu mno
miongoni mwa wale wanaochukia amani.
7Mimi ni mtu wa amani;
lakini ninaposema, wao wanataka vita.