The chat will start when you send the first message.
1Kama Mwenyezi Mungu hangekuwa upande wetu;
Israeli na aseme sasa:
2kama Mwenyezi Mungu hangekuwa upande wetu,
watu walipotushambulia,
3hasira yao ilipowaka dhidi yetu,
wangetumeza tukiwa hai,
4mafuriko yangegharikisha,
maji mengi yangetufunika,
5maji yaendayo kasi
yangetuchukua.
6Ahimidiwe Mwenyezi Mungu,
ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.
7Tumeponyoka kama ndege
kutoka mtego wa mwindaji;
mtego umevunjika,
nasi tumeokoka.
8Msaada wetu ni katika jina la Mwenyezi Mungu,
Muumba wa mbingu na dunia.