The chat will start when you send the first message.
1Mwenyezi Mungu alipowarejesha mateka Sayuni,
tulikuwa kama watu walioota ndoto.
2Vinywa vyetu vilijaa kicheko,
ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.
Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,
“Mwenyezi Mungu amewatendea mambo makuu.”
3Mwenyezi Mungu ametutendea mambo makuu,
nasi tumejaa furaha.
4Ee Mwenyezi Mungu, turejeshee watu wetu waliotekwa,
kama vijito katika Negebu.
5Wapandao kwa machozi
watavuna kwa nyimbo za shangwe.
6Yeye azichukuaye mbegu zake
kwenda kupanda, huku akilia,
atarudi kwa nyimbo za shangwe,
akichukua miganda ya mavuno yake.