The chat will start when you send the first message.
1Bwana ndiye mchungaji wangu,
sitapungukiwa na kitu.
2Hunilaza katika malisho
ya majani mabichi,
kando ya maji matulivu huniongoza,
3hunihuisha nafsi yangu.
Huniongoza katika njia za haki
kwa ajili ya jina lake.
4Hata nikipita katikati
ya bonde la uvuli wa mauti,
sitaogopa mabaya,
kwa maana wewe upo pamoja nami;
fimbo yako na mkongojo wako
vyanifariji.
5Waandaa meza mbele yangu
machoni pa adui zangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
kikombe changu kinafurika.
6Hakika wema na upendo vitanifuata
siku zote za maisha yangu,
nami nitakaa nyumbani mwa Bwana
milele.